Bunda FM Radio
Bunda FM Radio
November 28, 2025, 7:38 pm

”Nashauri kamati ya mikopo kujua historia za wakopaji hasa kwa wakopaji wageni ili kuepuka wakopaji kutokomea na fedha za chama”Shukrani Modest Mihungo Afisa ushrika Bunda mji
Na Amos Marwa
Wanachama wa chama cha ushirika wa akiba na mikopo cha Kibara biashara (SACCOS) wametakiwa kujiwekea akiba na hisa kwa wingi ili kupunguza tatizo la upungufu wa mitaji katika chama chicho.
Hayo yamebainishwa na Shukrani Modest Mihungo afisa wa vyama vya ushirika Bunda mji alie kuwa mgeni rasmi katika mkutano wa mwaka wa chama hicho kilichofanyika katika ukumbi wa Bunda fm radio na kusema kuwa kila mwanachama anatakiwa kuwa na utamaduni wa kujiwekea akiba na hisa mara kwa mara ili kukuza chama hicho na kupunguza tatizo hilo la upungufu wa mitaji.

Awali akisoma taarifa ya chama hicho wakati wa ufunguzi wa mkutano mkuu makamu mwenyekiti Hamadi Nyamanda amesema kuwa SACCOS hiyo inakabiliwa na chamangamoto lukuki lakini upungufu wa mitaji ndio kikwazo kikubwa cha maendeleo katika SACCOS hiyo
Kwa upande wao wanachama walioshiriki mkutano huo wamesema chama hicho kimekua faida kubwa kwao na kuahidi kuwa wataongeza hisa na kukopa kwa wingi ili kupunguza tatizo la uhaba wa mitaji

Mzee Barton Baraga mmoja wa wanachama wa chama cha chama cha ushirika wa akiba na mikopo cha Kibara biashara (SACCOS) akichangia hoja katika mkutano mkuu wa chama hicho. Picha na Amos Marwa
Mkutano huo wa 18 wa chama cha ushirika wa akiba na mikopo cha Kibara biashara (SACCOS) umeazimia kuwashirikisha wadau mbalimbali wa maendeleo kushirikiana na chama hicho huku kamati za ukopeshaji zikiweka mikakati kwa wakopaji wasio lipa kwa wakati kwa kuwafikisha katika vyombo vya sheria.