Bunda FM Radio
Bunda FM Radio
November 21, 2025, 10:21 am

Frank Gasper Mhina afisa kutoka mamlaka ya dawa na vifaa tiba kanda ya ziwa (TMDA) akitoa elimu juu ya visababishi na athari za usugu wa vimelea vya magonjwa dhidi ya dawa linalofahamika kama UVIDA. kwa wanafunzi wa chuo cha uwalimu Bunda. picha na Amos Marwa
”Tunatoa rai kwa wauzaji wa maduka ya madawa kuzingatia kutoa dawa sahihi na zilizosajiliwa na Mamlaka ya dawa na vifaa tiba (TMDA) ilikuondokana na usugu wa vimelea vya magonjwa dhidi ya dawa” Frank Gasper Mhini afisa kutoka mamlaka ya dawa na vifaa tiba kanda ya ziwa (TMDA)
Na Amos Marwa
Jamii imeaswa kuacha matumizi ya dawa kiholela bila kufuata taritibu za kitabibu ili kuepukana na tatizo la usugu wa vimelea vya magonjwa dhidi ya dawa linalofahamika kama UVIDA.
Hayo yamebainishwa Frank Gasper Mhini afisa kutoka mamlaka ya dawa na vifaa tiba kanda ya ziwa (TMDA) wakati akitoa elimu ya matumizi sahihi ya dawa iliyofanyika chuo Cha uwalimu Bunda na kusema kuwa ni lazima kufuata maelekezo ya kitabibu ili kutumia dawa kwa matumizi sahihi kuepuka janga la UVIDA.
Mhini amesema kama jamii haitazingatia matumizi sahihi ya dawa gharama za matibabu zitakuwa juu na vimelea vya magonjwa vitakuwa sugu na kusababisha kifo kwa mtumiaji

Wanafunzi wa chuo cha uwalimu Bunda wakifuatilia kwa ukaribu mafunzo yanayotolewa na mamlaka ya dawa na vifaa Tanzania (TMDA). picha na Amos Marwa
Kwa upande wao washiriki wa mafunzo hayo wamesema elimu hiyo itawasadia kuepukana na UVIDA na kuomba elimu hiyo kutoka TMDA kuwa endelevu.
Mamlaka ya dawa na vifaa tiba (TMDA)imewataka wamiliki wa maduka ya dawa za binadamu kuuza dawa zenye ubora na zilizosajiliwa na (TMDA) ilikuondokana na usugu wa vimelea vya magonjwa dhidi ya dawa linalofahamika kama UVIDA.
