Bunda FM Radio
Bunda FM Radio
November 13, 2025, 5:33 pm

”Nawaomba wakulima wote kujiunga kwenye mtandao wa vikundi vya wakulima Tanzania (MVIWATA) ili waweze kuwa na sifa za kukopeshwa pembejeo za kilimo” Benard Mathew afisa kilimo kata ya Bunda stoo
Na Amos Marwa
Wakulima wadogowagogo mkoa wa Mara wamehakikishiwa fursa za masoko na upatikanaji wa mbegu za ruzuku ili kuimarisha maslahi yao. Hayo yamebainishwa na Benard Mathew afisa kilimo kata ya Bunda stoo aliekuwa mgeni rasmi kwa niaba ya Afisa kilimo wilaya ya Bunda kwenye mkutano wa mtandao wa vikundi vya wakulima Tanzania (MVIWATA) Kwa mkoa wa Mara uliofanyika ukumbi wa vileji wilaya ya Bunda na kusema kuwa serikali kupitia wizara ya kilimo itatoa mbegu za ruzuku, viwatilifu na masoko ya uhakika ili kuleta tija kwa wakulima.
Hayo yamebainishwa na Benard Mathew afisa kilimo kata ya Bunda stoo aliekuwa mgeni rasmi kwa niaba ya Afisa kilimo wilaya ya Bunda kwenye mkutano wa mtandao wa vikundi vya wakulima Tanzania (MVIWATA) Kwa mkoa wa Mara uliofanyika ukumbi wa vileji wilaya ya Bunda na kusema kuwa serikali kupitia wizara ya kilimo imetoa mbegu za ruzuku, viwatilifu na masoko ya uhakika ili kuleta tija kwa wakulima
Akisoma taarifa katibu wa MVIWATA mkoa wa Mara Baraka Sagare amesema lengo la chombo hicho ni kuwezesha mawasiliano miongoni mwa wakulima wadogo wadogo ili kujenga ushawishi na utetezi kwa manufaa ya wakulima hao
Mtandao wa vikundi vya wakulima Tanzania(MVIWATA) umeanzishwa kwaka 1993 ikiwa ni chombo kinachowaunganisha wakulima wadogowadogo na kutengeneza sauti moja.
