Bunda FM Radio
Bunda FM Radio
November 12, 2025, 8:50 pm

Katibu wa Mtandao wa vikundi vya wakulima Tanzania (MVIWATA) Mkoa wa Mara akizungumza na Bunda FM kwenye kipindi cha Busati la Habari kinachoruka Jumatatu hadi Ijumaa. Picha na Amos Marwa
“MVIWATA inawapa nafasi wakulima wadogowadogo kujifunza kilimo bora kwa kupewa elimu tunafanya shughuli hizi tukiwa na wataalamu wa kilimo hivyo wakulima kupitia vikundi vyao wanajifunza ni zipi mbegu sahihi na njia sahihi za kilimo chenye tija’’ Baraka Sagare katibu wa Mtandao wa vikundi vya wakulima mkoa wa mara (MVIWATA).
Na Amos Marwa
Wakulima wadogowadogo mkoa wa Mara wametakiwa kujiunga katika Mtandao wa vikundi vya wakulima Tanzania (MVIWATA). Ili kuweza kulima kwa tija na kuondokana na kilimo holela.
Hayo yamebainishwa na Baraka Sagare katibu wa Mtandao wa vikundi vya wakulima mkoa wa mara (MVIWATA). wakati akizungumza na Bunda FM katika kipindi cha Busati la Habari na kusema kuwa kupitia chombo hicho wakulima watapewa elimu na wataalamu ili kuweza kulima kilimo chenye tija , ameongeza kuwa pamoja na uwepo wa changamoto za mitaji na upatikanaji wa mbegu bora lakini chombo hicho kimekuwa sauti imara ya kuwasemea wakulima na kulinda haki zao ikiwemo bei na masoko ya kuuzia bidhaa zao hivyo kuwaomba wakulima wote ambao sio wanachama kutumia mkutano utakao fanyika novemba 13, 2025 wilaya ya Bunda kujiunga kwa kingilio cha Tsh 5,000 ili kuwa wanachama wa chombo hicho.