Bunda FM Radio
Bunda FM Radio
October 27, 2025, 9:24 pm

Mkuu wa polisi wilaya ya Butiama(OCD) Mrakibu mwandamizi wa jeshi la polisi Daudi Methew Ibrahim akizungumza na Bunda FM kwenye kipindi cha Busati la Habari kinachoruka Jumatatu hadi Ijumaa. Picha na Witness Joseph
’Wananchi wajitokeze kwa wingi kupiga kura wakiwa na ari butiama kutakuwa shwari na salama kabisa na baada ya kupiga kura warudi nyumbani kusubiri matokeo’’Mkuu wa polisi wilaya ya Butiama(OCD)Mrakibu mwandamizi wa polisi Daudi Methew Ibrahim
Na Amos Marwa
Wananchi wilaya ya Butiama wamehimizwa kujitokeza kushiriki uchaguzi mkuu kwa amani na utulivu na kurejea majumbani kwao kwa ajili ya kusubiri michakato ya matokeo ya uchaguzi.
Hayo yamebainishwa na Mkuu wa polisi wilaya ya Butiama(OCD) Mrakibu Mwandamizi wa jeshi la polisi Daudi Methew Ibrahim wakati akizungumza na Bunda FM katika kipindi cha Busati la Habari na kusema kuwa wananchi hawana wajibu wa kulinda kura hivyo baada ya kupiga kura wanapaswa kurejea majumbani kwendelea na shughuli zao, ameongeza kuwa mpaka sasa hakuna tishio lolote wala kikundi chochote kilichopanga kufanya uvunjifu wa amani siku ya uchaguzi mkuu.