Bunda FM Radio

Wananchi Mara wahimizwa kulinda amani kuelekea uchaguzi mkuu

October 16, 2025, 12:37 pm

Mkuu wa polisi wilaya ya Butiama(OCD) Mrakibu mwandamizi wa jeshi la polisi Daudi Methew Ibrahim akizungumza na Bunda FM kwenye kipindi cha Busati la Habari kinachoruka Jumatatu hadi Ijumaa. Picha na Witness Joseph

Nchi yoyote ili iwe na maendeleo ni lazima kuwepo na amanai na utulivu hivyo kila mtu anawajibu wa kulinda tunu hii ya amani”Mkuu wa polisi wilaya ya Butiama(OCD)rakibu mwandamizi wa polisi Daudi Methew Ibrahim

Na Amos Marwa

Wananchi mkoa wa Mara wahimizwa kulinda na kuimarisha amani utulivu na usalama katika kipindi cha uchaguzi na baada ya uchaguzi mkuu.

Hayo yamebainishwa na Mkuu wa polisi wilaya ya Butiama(OCD) Mrakibu Mwandamizi wa jeshi la polisi Daudi Methew Ibrahim wakati  akizungumza na Bunda FM katika kipindi cha Busati la Habari na kusema kuwa tunapaswa kukumbatia amani tuliyonayo ili twendelee kulijenga taifa letu kiuchumi na kuongeza kuwa kama amani itavurugwa watu hawatapata nafasi ya kujihusisha na uzalishaji mali badala yake watakuwa wakikimbia machafuko.