Bunda FM Radio
Bunda FM Radio
October 3, 2025, 3:16 pm

”Shule yetu inakabiliwa na uhaba wa Walimu na upungufu wa Maabara jambo linalofanya tushindwe kujifunza masomo yetu kwa ufanisi” maneno ambayo ni sehemu ya risala kidato cha nne Bunda stoo Sekondari.
Na Amos Marwa
Wadau mbambali wa elimu wametakiwa kushirikiana ili kuondoa changamoto ya upungufu wa Walimu uliopo katika shule ya sekondari Bunda stoo na shule zingine zilizopo halmashauri ya mji wa Bunda.
Rai hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Mtaa wa Idara ya maji Mtaki Bwire aliekuwa mgeni rasmi katika hafla ya mahafari ya pili ya kidato cha nne katika shule ya sekondari Bunda stoo yaliyofanyika katika viwanja vya shule hiyo na kuwaomba Afisa elimu kata na Afisa elimu sekondari kuwasilisha uhitaji wa walimu kwa mkurugenzi wa Mji wa Bunda ili kuondoa changamoto hiyo ikiwa ni sehemu ya kujibu risala iliyosomwa na wa hitimu wa shule hiyo.

Kwa upande wa Mwalikishi wa wazazi wa wahitimu Noella Richard amewashukuru Walimu kwa kuwalea watoto wao kwa madili mema kwa miaka minne na kuwataka wahitimu hao kutumia maadili hayo katika jamii.

Nao wahitimu wa mahafari hayo wamewashukuru walimu kwa ushirikiano wao katika safari ya miaka mi nne na kuahidi kuwa watafanya vizuri katika mitihani yao itakayofanyika novemba mwaka huu.
Sauti za wahitimu wakitoa shukrani zao kwa Walimu kwa ushirikiano wa pamoja kwa miaka minne na kuelezea maandalizi yao kwelekea mitihani yao ya kidato cha nne itakayofanyika novemba mwaka huu.

Jumla ya wahitimu 333 katika shule ya sekondari Bunda stoo wanatarajia kuingia katika mitihani ya kidato cha nne 2025 ikiwa wavulana ni 178 na wasichana 155 .