Bunda FM Radio
Bunda FM Radio
September 11, 2025, 9:01 pm

“Kila mwana Mara anawajibu wa kutunza bonde la Mto Mara na hifadhi nyingine kwa ajili ya maendeleo yetu na vizazi vijavyo ‘’ Mkuu wa mkoa wa Mara Kanali Evans Alfred Mtambi.
Na Amos Marwa
Mkuu wa mkoa wa Mara Kanali Evance Alfred Mtambi amewataka wananchi na wadau mbalimbali kujitokeza kwa wingi katika Maadhimisho ya 14 ya bonde la Mto Mara yanayofahamika kama siku ya mara (Mara Day) yatakayofanyika septemba 12 na kuhitimishwa septemba 15 katika uwanja wa Mwenge Butiama .
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Mtambi amesema lengo la Maadhimisho hayo ni kutoa elimu ya uhifadhi wa bonde la Mto Mara unaohusisha milima mito ,mabonde na mapori liloanzia milima ya mawe nchini Kenya na kuishia ziwa Viktoria nchini Tanzania.
Ameongeza kuwa Bonde la mto mara linachangia na kuwa chachu ya kuhifandhi hifadhi ya taifa ya serengeti na kufanya hifadhi hiyo kuwa Bora na kushuhudiwa uhamaji wa wanyama na kufanya hifadhi ya serengeti kuwa hifadhi Bora barani Afrika kwa vipindi viwili mfululizo.
Maadhimisho ya siku ya Mara kwa mwaka 2025 yaliyobeba kauli mbiu isemayo “Hifadhi Mto Mara linda Uhai” yatahusisha shughuli mbalimbali za uhifadhi ikiwemo upandaji miti zaidi ya 8,000 katika vijiji vinavyopakana na Mto Mara, Kongamano la kisayansi litakalofanyika chuo kikuu Cha Mwalimu Nyerere huku burudani ya michezo mbali mbali ikiwemo kufukuza kuku, Mbio fupi, kukumbia kwenye magunia , kuvuta kamba ikichagiza maadhimisho hayo.