Bunda FM Radio
Bunda FM Radio
August 28, 2025, 5:00 pm

”Vijana tunaweza kuleta mabadiliko makubwa kupitia siasa nakusihi kijana mwenzangu usiogope usikate tamaa siasa sio lazima uwe na pesa kama wengi mnavodhani ni kujitoa na kujiamini” Lucas Daniel Marco maarufu kama Three Boys, kijana mwanasiasa na mgombea udiwani kata ya Nyamakokoto Bunda Mji kupitia chama cha mapinduzi (CCM)
Na Amos Marwa
Vijana wilayani Bunda wameaswa kujitosa kwenye siasa ili kuiletea jamii maendeleo.
Hayo yamebainishwa na Lucas Daniel Marco maarufu kama Three Boys, kijana mwanasiasa na mgombea udiwani kata ya Nyamakokoto Bunda Mji kupitia chama cha mapinduzi (CCM) wakati akizungumza na Bunda FM katika kipindi cha Busati la Habari na kusema kuwa vijana wanauwezo wa kuiletea jamii maendeleo kwani wana nguvu ya kufanya kazi na kuwatumikia wananchi hivyo vijana kujitokeza katika siasa bila uoga.