Bunda FM Radio

Jamii Mara yaaswa kutunza na kuenzi tamaduni

August 20, 2025, 7:52 pm

Maringo Ndolela aliekaa kulia na Felix Lukonge Sola wawakilishi wa koo za kabila la wajita wakizungumza na Bunda FM kwenye kipindi cha Busati la Habari kinachoruka Jumatatu hadi Ijumaa. Picha na Amos Marwa

”Nawakaribisha Wajita wote na makabila mengine kutoka mkoa wa Mara wafike katika tamasha la kuenzi mira na tamaduni za kijita ili waone uhalisia uliopo maana tunataka kurudisha tamaduni nzuri za zamani ili ziweze kutumika sasa”Felix Lukonge Sola mwakilishi wa koo za kabila la wajita.

Na Amos marwa

Jamii mkoa wa Mara imeaswa kutunza, kuenzi na kwendeleza tamaduni ili kudumisha asili na kulinda maadali ya watoto.

Hayo yamebainishwa na Maringo Ndolela na Felix Lukonge Sola wawakilishi wa koo za kabila la wajita wakati wakizungumza na Bunda FM katika kipindi cha Busati la Habari na kuwataka wajita na makabira mengine mkoa wa mara kujitokeza kwa wingi katika tamasha la kuenzi mira na tamaduni za kijita litakalofanyika agosti 22, 2025 katika kijiji cha Bukima wilaya ya musoma vijijini yenye lengo la kuendeleza mira na tamaduni nzuri kwa jamii ambalo limeandaliwa na Chifu wa wajita Profesa Charles Lukiko Majinge Tamasha hilo litahususisha burudani mbalimbali kutoka kwa wasanii akiwemo msanii pendwa wa kabili hilo Maringo Ndolela na michezo mingine ambapo washindi watakabidhiwa zawadi zao na Mkuu wa mkoa wa Mara kanali Evans Alfred Mtambi anaetarajiwa kuwa mgeni rasmi wa tamasha hilo.