Bunda FM Radio
Bunda FM Radio
August 13, 2025, 6:04 pm

”Tukumbuke kuwa mwenge wa uhuru huleta tumaini pasipo tumaini, upendo palipo na chuki ”Mkuu wa mkoa wa Mara Kanali Evans Alfred Mtambi.
Na Amos Marwa
MKuu wa mkoa wa Mara Kanali Evans Alfred Mtambi amewataka wananchi na wadau wote kujitokeza kwa wingi kushiriki mbio za mwenge wa uhuru kwa kipindi chote mwenge utakapo kuwa mkoa wa Mara.
Akizungumza na wandishi wa habari Mtambi amesema kuwa mkoa wa Mara utapokea mwenge wa uhuru kutoka mkoa wa Simiyu agosti 15, 2025 na mapokezi hayo yatafanyika katika uwanja wa shule ya msingi Balili.
Ameongeza kuwa agosti 15 mwenge wa uhuru utaanza kukimbizwa katika Halmashauri ya mji wa Bunda na kupitia Halmashauri zote 9 za mkoa Mara na kuhitimisha mbio hizo agosti 23 katika Halmashauri ya wilaya ya Bunda.
Mwenge wa uhuru ukiwa Mkoa wa Mara utakimbizwa jumla ya kilometa 1,123 ukitembelea , kukagua, kuweka mawe ya Msingi, kufungua na kuzindua jumla ya miradi 68 ya maendeleo yenye thamani ya jumla shilingi bilioni 26.54.