Bunda FM Radio
Bunda FM Radio
August 10, 2025, 8:22 pm

“Mimi Janeth naamini katika kutoa katika mizunguko yangu yote naamini ukimtolea Bwana unabarikiwa zaidi tujifunze kutoa kwa moyo tuone baraka za Bwana zinavomiminika”Mkurugenzi wa kampuni ya Janeth Moters Janeth Webiro
Na Amos Marwa
Kampuni ya Janeth Motors limited inayojishughulisha na uuzaji wa magari, pikipiki, upimaji na uzaji wa viwanja imetoa vifaa vya Mziki Maiki 5 na kiasi cha pesa za kitanzania Laki Tatu katika kanisa la AICT Changuge kwenye hafla ya Changizo iliyofanyika katika kanisa hilo ikiwa ni sehemu ya kurudisha kwa jamii.
Akizungumza katika hafla hiyo Mkurugenzi wa kampuni hiyo Janeth Webiro aliekuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo amesema kumtolea Mungu ni sehemu ya Baraka na mafanikio.

Meneja wa Kampuni ya hiyo Waiter Natay amesema biashara na imani vinaendana hivyo kampuni hiyo imejitolea kushirikiana na jamii kwa ajili ya maendeleo.
Kwa upande wao viongozi wa kanisa la AICT Changuge wamesema vifaa hivyo vitasaidia kanisa hilo kueneza injili na kuishukuru kampuni ya Janeth Motors na kuwataka kuwa na moyo wa kwendelea kusaidia jamii.
Hafla hiyo ya Changizo imeandaliwa na idara ya wanawake Makanisa ya AICT Changuge, Kisangwa, Mirungu na Bukore kutoka kata ya Mcharo kwa ajili ya kupata michango ya kweneza utume na kuendeleza kanisa hilo.
