Bunda FM Radio

 TCRA Kanda ya Ziwa yatoa elimu uhakiki wa vyanzo vya habari

July 28, 2025, 7:30 pm

Afisa Mawasiliano TCRA Kanda ya Ziwa Bernadetha Clement Mathayo akizungumza na Bunda FM kwenye kipindi cha Busati la Habari kinachoruka Jumatatu hadi Ijumaa. Picha na Amos Marwa

Wananchi mnapaswa kutumia mitandao ya kijamii kama fursa ya kutangaza biashara zenu na siyo kupoteza muda kwa kuangalia habari  za udaku muda wote’’  Bernadetha Clement Mathayo Afisa Mawasiliano TCRA kanda ya ziwa.

Na Revocutus Andrew

Wananchi Kanda ya Ziwa wameaswa kuwa na tabia ya kuhakiki vyanzo vya habari wanazopata kwenye mitandao ya kijamii ili kuwa na uhakika wa habari hizo kabla ya kuzitumia au kuzisambaza kwa watu wengine.

Hayo yamebainishwa na Afisa Mawasiliano wa TCRA kanda ya ziwa Bernadetha Clement Mathayo wakati akizungumza na Bunda FM katika kipindi cha Busati la Habari kuhusu kampeni mpya ya futa delete kabisa. Ameongeza kwa kusema lengo la kampeni hiyo ni kuwawezesha wananchi kutotenda kosa la kusambaza taarifa zisizo sahihi na za upotoshaji.