Bunda FM Radio
Bunda FM Radio
July 26, 2025, 10:13 am

“Mkatumie mikopo hii kwa lengo lilopangwa ili muweze kurejesha kwa wakati ili vikundi vingine vikanufaike na mikopo hii hatutegemie kuwaona katika kumbi za staarehe kama baa mkinywa bia kutumia fedhaa hizi za mikopo” Katibu tawala Wilaya ya Bunda Salmu Alfan Mtelela
Na Amos Marwa
Vikundi vya akina mama, Vijana na wenye ulemavu wilaya ya Bunda wametakiwa kutumia fedha za mikopo inayotolewa na Halmashauri kwa lengo lilokusudiwa ili kusaidia vikundi hivyo kuondokana na hali ya umasikini.
Hayo yamebainishwa na Katibu tawala Wilaya Bunda Salmu Khalfan Mtelela aliekuwa mgeni rasmi wakati wa hafla ya kukabidhi Hundi ya shilingi milioni 435.2 , pikipiki 8 na bajaji 2 kwa vikundi hivyo iliyofanyika katika ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya mji wa Bunda.
Kwa upande wao wenyeviti wa vikundi hivyo wamesema mikopo hiyo isiyokuwa na riba itawasaidia kujikwamua kimaisha na kuishukuru serikali kwa kutoka mikopo hiyo ya asilimia kumi ya mapato ya ndani ya halmashauri.

Mikopo hiyo ya asilimia 10 ambayo inatolewa na Serikali ni sehemu ya kuimarisha maendeleo kwa jamii na kuepusha makundi hayo kuingia katika mikopo yenye riba kubwa.
