Bunda FM Radio

Tanesco: Upatikanaji wa umeme Mara unaridhisha

July 25, 2025, 3:08 pm

Meneja wa Tanesco mkoa wa Mara Injinia Nikson Babu akizungumza na Bunda Fm kwenye kipindi cha ukurasa mpya. Picha na Amos Marwa

”Jumapili tarehe 27/7/2025 kuanzia saa 4 asubuhi mpaka saa 8 mchana wateja na wananchi wote katika mikoa ya Mwanza na Mara watashuhudia tukio la kukosekana kwa umeme hadi katika ofisi za Tanesco kwa sababu kituo kikuu kinachopokea umeme kanda ya ziwa kilichopo mkoani Shinyanga kitazimwa kwa ajili ya matengenezo muhimu’ Injinia Nikson Babu Meneja wa Tanesco mkoa wa Mara.

Na Revocatus Andrew

Shughuli za maendeleo zinaendelea kukua vizuri mkoani Mara kwasababu upatikanaji na matumizi ya umeme mkoani Mara ni shwari na wa kuridhisha.

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa Tanesco mkoa wa Mara Injinia Nikson Babu wakati akizungumza na Bunda fm kupitia kipindi cha ukurasa mpya wakati akielezea hali ya upatikanaji wa umeme katika mkoa Mara. Ameongeza kuwa katika uboreshaji na upatikanaji wa umeme mkoani Mara kutakuwa na matengenezo ya Transfoma kubwa zinazo safirisha umeme kwa siku mbili jumamosi na jumapili tarehe 26 na 27 hivyo kutakuwa na mgao wa umeme kwa baadhi ya maeneo na hivyo kuwaomba wananchi kuwa wavumilivu kwani maboresho hayo yanalengo la kuongeza upatikanaji wa umeme.