Bunda FM Radio

Wadau wa jukwaa la kilimo Bunda washauriwa kutoa elimu kwa Wakulima

June 26, 2025, 12:55 pm

Viongozi wa jukwaa la Wakulima Bunda. Picha na Revocatus Endrew

“Tusikae na kujadili na kuishia kwenye vikao maana itakuwa ni kama hadithi tu inabinidi tunde kwa wakulima na kuwashawishi wa kulima kwa ajili ya kilomo chenye tija”. Mwenyekiti wa jukwaa la wakulima Mashaka Charles

na Revocatus Endrew

Wadau wa jukwaa la kilimo wilaya ya bunda wameshauriwa kuyafanyia kazi yote wanayokubaliana katika vikao vyao.

Akizungumza katika jukwaa hilo hii leo mwenyekiti wa jukwaa hilo Bwana mashaka Charles amesema si vyema wajukwaaa kuwa nyuma katika maswala ya kilimo hasa upimaji wa afya ya Udongo.

Sauti ya Mwenyekiti wa jukwaa la wakulima Mashaka Charles akiwaasa wadauu wa jukwaa la kilimo kuwafikia wakulima

Baraka Kamese Mratibu wa shirika lisilo la kiserikali Bufadeso. Picha na Revocatus Endrew

Kwa upande wake Diwani wa kata ya kunzugu Pasaka Shabani Samsoni amesema kuna faida kubwa sana katika kupima afya ya udongo kwan hata yeye ameona faida zake

Akichangia mjadala huo Victor Ulomi Afisa miradi toka Shirika lisilo la kiserikali la bufadeso amesema upo umuhimu mkubwa wa kupima afya ya udongo kwani huongeza pato kwa wakulima

Sauti ya Victor Ulomi Afisa miradi toka Shirika lisilo la kiserikali la bufadeso akielezea umuhimu wa kupima afya ya udongo na faida zake.

Jukwaa hilo la wakulima Bunda hufanyika mara tatu kwa mwaka chini ya ufadhili ya shirika lisilo la kiserika la BUFADESO lenye ofisi zake katika kata ya kunzugu wilaya ya bunda mkoani Mara.

Victor Ulomi Afisa miradi toka Shirika lisilo la kiserikali la bufadeso. Picha na Revocatus Endrew