Bunda FM Radio
Bunda FM Radio
June 20, 2025, 6:12 pm

“Vijiji vyote vilivyopitiwa na mradi wa maji ikiwemo Bisarye, Nyamswa,Ikizu na Bukama vinufaike na mradi ili kupunguza uharibifu kwa miundombinu ya maji kwa vijiji ambavyo sio wanufaika” Joshua Mirumbe Mwenyekiti wa Bodi ya Maji Wilaya ya Bunda
Na Amos Marwa
Mwenyekiti wa Bodi ya maji wilaya ya Bunda Joshua Mirumbe amewataka wakala wa Maji na usafi wa mazingira (BUWASSA)kuongeza kasi ya utekelezaji wa Mradi wa Maji wa Mgango-Kiabakari ili wananchi waweze kupata huduma ya maji kwa wakati.
Mirumbe ameyasema hayo alipokagua mradio huo wenye thamani ya bilioni 80.3 na kusema kuwa wananchi wanahitaji maji kwa haraka na kuongeza kuwa vijiji vilivyopitiwa na mradi watanufaika na maji ikiwemo Bisarye, Nyamswa na Ikizu.

Kaimu Mkurugenzi wa Wakala wa maji safi na usafi wa mazingira Bunda (BUWASSA), Daudi Ashraf akielezea hatua ya utekelezaji wa mradi wa maji wa Mgango-Kiabakari. Picha na Amos Marwa
Nae, kaimu Mkurugenzi wa Wakala wa maji safi na usafi wa mazingira (BUWASSA), Daudi Ashraf amesema kuwa mradi huo umeanza Februari mwaka huu na umetekelezwa kwa asilimia 15 na unatarajiwa kukamilika mwezi januari ,2026.

Wananchi wa kata ya Nyamswa ambapo mradi huo umepita wamesema kukamilika kwa mradi kutawasaidia kuondokana na adha ya Maji ambayo imekuwa kilio chao cha muda mrefu.
Mradi huo wa Mgango-Kiabakari Utagharimu jumla ya bilioni 80.3 mpaka kukamilika huku ukitarajia kunufaisha zaidi ya wananchi 51,000.
