Wajumbe wa kamati ya maendeleo ya kata ya Bunda stoo halmashauri mji Bunda wampongeza Diwani
Wajumbe wa kamati ya maendeleo ya kata ya Bunda stoo halmashauri mji Bunda wampongeza Diwani
June 11, 2025, 10:52 am
Diwani wa kata ya Bunda stoo Flavian Chacha Nyamigeko akipokea Keki iliyoandaliwa na Wajumbe wa kamati ya Maendeleo ya kata hiyo. Picha na Amos Marwa
“Hakuna sehemu ambayo miradi haijakamilika kwa kipindi cha miaka mitano miradi ya hospitali tumepeleka fedha na mitaa yote mitano iliyopo ndani ya kata ya Bunda stoo tumepeleka maji ” Flaviani Chacha Nyamigeko Diwani kata ya Bunda stoo.
Na Amos Marwa
Kata ya Bunda stoo Halmashauri ya Mji wa Bunda imetumia kiasi cha fedha zaidi ya shiling bilion 5.7 katika utekelezaji wa miradi ikiwemo hospitali ya mji wa Bunda, ujenzi wa shule ya msingi Miembeni, miradi ya maji, madaraja na miundombinu ya barabara kwa Mwaka 2021-2025.
Hayo yamebainishwa na diwani wa kata hiyo Flaviani Chacha Nyamigeko wakati akizungumza na wajumbe wa kamati ya maendeleo wa kata ya Bunda stoo kwenye hafla fupi ya kumpongeza diwani katika kipindi chote cha uongozi wa miaka mitano
Sauti ya diwani wa kata ya Bunda stoo Flaviani Chacha Nyamigeko akielezea kiasi cha fedha na jumla ya miradi iliyotekelezwa kwa mwaka 2021-2025Wajumbe wa kamati ya Maendeleo kata ya Bunda stoo wakisikiliza taarifa ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa mwaka 2021-2025 . Picha na Amos Marwa
Nae diwani wa kata ya Manyamanyama Yohana Machilu amesema mahusiano mazuri aliyonayo diwani wa kata ya Bunda stoo na wadau mbali mbali wa maendeleo kumesaidia kutekeleza miradi kwa wakati.
Sauti ya Diwani wa kata ya Manyamanyama Yohana Machilu akielezea jinsi mahusiano mazuri aliyonayo diwani wa kata ya Bunda stoo na wadau wa maendeleoa imesaidia kutekeleza miradi ya maendeleo kwa wakati Mwenyekiti wa Mtaa wa Butakale Sebastiani Chacha Masubo akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa miradi ikiwemo sekta ya elimu , miundombinu ya barabara, maji na afya kwa mwaka 2021-2025 kwa wajumbe wa kamati ya maendeleo na viongozi wa chama cha Mapinduzi (CCM). Picha na Amos Marwa
Kamati hiyo ya Maendeleo imemzawadia diwani huyo zawadi mbali mbali ikiwemo suti, viatu na blanketi ikiwa ni kuthamini mchango wa kazi yake ndani ya miaka mitano.
Wajumbe wa kamati ya maendeleo na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kata ya Bunda stoo wakiongozwa na diwani wa kata hiyo Flaviani Chacha Nyamigeko wakipata chakula Cha mchana kwenye hafla fupi kumpongeza diwani huyo. Picha na Amos Marwa