Bunda FM Radio
Bunda FM Radio
May 21, 2025, 11:20 am

”Siasa ni maisha lazima tuchague viongozi wanaokuwa karibu na wananchi na wanaojuwa maisha ya wananchi wanaowaongoza”, maoni ya mwananchi wilayani Bunda.
Na Amos Marwa
Wananchi Wilayani Bunda wamesema kueelekea Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Octoba mwaka huu wamejipanga kuchagua Viongozi waadilifu, wasio kula Rushwa na wanaojuwa changamato zao.
Wakizungumza na BUNDA FM, Wananchi hao wamesema kumekuwa na Tabia ya baadhi ya Viongoziamabao sio waadilifu, hawapo karibu na Wananchi katika kutatua kero zao na kuahidi kuwa uchaguzi wa mwaka huu watachagua Viongozi waadilifu na wenye kuwaletea maendeleo.
Uchaguzi mkuu unatarajiwa kufanyika Octoba 25, 2025 kotenchini ili kupata Madiwani, Wabunge na Rais watakao kuwa madarakani kwa miaka mitano ijayo kwa mujbu wa katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.
