Bunda FM Radio
Bunda FM Radio
April 23, 2025, 2:49 pm

Wafanyabiashara wengi wilayani Bunda kupata fursa ya kuongeza vipato vyao kwa kuongezwa ukubwa wa soko
Na Adolf Mwolo
Zaidi ya shilingi milioni 900 zinatarajiwa kutumika kukarabati soko la Manjebe lililoko kata ya Nyasura wilaya ya Bunda mkoani Mara.
Akizungumza na Bunda fm Radio Diwani wa kata hiyo Samweli Kiboko amesema kuboreshwa kwa soko hilo kutaongeza kipato katika kata hiyo na kwa wafanya biashara wa bidhaa za jumla wa mkoa wa Mara na jamii kwa ujumla.