Bunda FM Radio
Bunda FM Radio
April 23, 2025, 10:28 am

Wakulima wameshauriwa kuwa na utaratibu wa kupima afya ya udongo kabla msimu wa kilimo kuanza
Na.Revocutus Andrew
Wakulima nchini wametakiwa kupima afya ya udongo pamoja na kulima kilimo asilia.
Hayo yamezungumzwa Leo na Bensoni Mturi afisa Teknolonjia za kilimo kutoka Halmashauri ya wilaya ya Bunda katika kikao Cha jukwaa la wadau wa kilimo “Development support organization (BUFADESO), kilichofanyika katika ukumbi wa Harieth uliopo katika Halmashauri ya wilaya ya Bunda mjini na kuwataka wakulima wote nchini kujenga tabia ya kupima udongo kabla ya kupanda mbegu za mazao Yao ili kuongeza ufanisi wa uzalishaji shambani na kukuza kilimo na vipato vya wakulima.
Mturi amesema wakulima wahakikishe wanatumia kilimo asilia na ikiwemo matumizi ya mbegu za asili, mbolea na dawa ili kuachana na mazoea ya kutumia dawa za kemikali kuua wadudu na mbolea za kisasa badala yake watumie dawa za asili Ili kuepukana na madhara yatokanayo na dawa za kisasa.