Bugaga wanufaisha na Miche 120,000 ya kahawa
Buha FM Radio

Bugaga wanufaika na Miche 120,000 ya kahawa

10/03/2026, 23:31

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu, Wakili Emmanuel Ladislaus akikabidhi mche wa kahawa kwa mwananchi wa Bugaga. Picha na Mwandishi wetu.

“Tungependa kahawa hii imee na kusambaa katika Halmashauri yetu ya Wilaya ya Kasulu, hivyo tumieni fursa hii ambayo serikali imeitoa bure mkaitunze na msiende kuifanyia biashara badala yake mkaipande kwenye maeneo yenu”Amesema Ladislaus.

Na; Mwandishi wetu

Wakazi wa Kijiji cha Bugaga na maeneo jirani wilayani Kasulu Mkoani Kigoma wamejitokeza kuchukua miche 120,000 ya kahawa aina ya Arabica iliyotolewa bure na Halmashauri ya Wilaya hiyo katika awamu ya pili ya ugawaji, ikiwa ni hatua ya kuongeza uzalishaji na kuimarisha uchumi wa wakulima.

Akizungumza wakati wa zoezi hilo kijijini hapo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu, Wakili Emmanuel Ladislaus, amesema ugawaji wa miche hiyo unaonesha dhamira ya serikali kuwasaidia wananchi kuimarisha uchumi wao kupitia kilimo.

Sauti ya Wakili Emmanuel Ladislaus.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu, Wakili Emmanuel Ladislaus akiwa anazungumza na wakazi wa Bugaga kulia ni Mkuu wa Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu, Mikidadi Mbaruku. Pisha na Mwandishi wetu.

Kwa upande wake, Mkuu wa Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu, Mikidadi Mbaruku, amesema hadi sasa jumla ya miche 420,000 ya kahawa tayari imeshasambazwa katika maeneo mbalimbali ya Halmashauri hiyo na kusema wataalamu wa kilimo wataendelea kutoa elimu kwa wakulima kuhusu namna bora ya kupanda na kuitunza miche hiyo.

Sauti ya Mikidadi Mbaruku.

Nao baadhi ya wananchi waliopokea miche hiyo akiwemo Peter Bisakala na Mariam Masoud , wameishukuru serikali kwa kuwapatia miche hiyo bure, wakisema hatua hiyo itawasaidia kuimarisha uchumi wao kwa kuanza kulima zao la kudumu badala ya kutegemea mazao ya muda mfupi.

Suti za wakazi wa Bugaga.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu, Wakili Emmanuel Ladislaus akikabidhi mche wa kahawa kwa mwananchi wa Bugaga Mariam Masoud. Picha na Mwandishi Wetu.