Buha FM Radio
Buha FM Radio
December 21, 2025, 7:25 pm

Watumishi wa hospitali ya rufaa Kabanga wamekutana kwa pamoja kusherehekea shelehe ya funga mwaka ilizoambatana na burudani mbalimbali na utunukiwaji wa vyeti kwa baadhi ya watumishi waliofanya vizuri katika idara zao kwa mwaka 20225.
Na; Sharifat Shinji
Hospitali ya rufaa Kabanga imewapongeza na kuwatunuku vyeti vya utumishi bora baadhi ya wafanya kazi wa hospitali hiyo iliyopo Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma lengo likiwa kuongeza hamasa ya utendaji kazi wa watumishi hao.
Pongezi hizo zimetolewa na Mganga mfawidhi wa hospitali hiyo Dakitari bingwa wa upasuaji Ndg. Peter Kitenyi wakati wa hafla ya kufunga mwaka 2025 iliyofanyika Jumamosi ya Desemba 20 katika ukumbi wa Bwami Dubai katika Halmashauri ya Mji Kasulu na kusema umekuwa mwaka wa mafanikio licha ya changamoto mbalimbali zilizojitokeza.
“Ndugu zangu kwanza tujipongeze mwaka umeisha salama tumefanya kazi kubwa sana licha ya changamoto za hapa na pale lakini Kabanga imebaki salama hivyo tuendelee kufanya kazi kwa ushirikiano”Amesema Dkt. Kitenyi.

Aidha Dkt. Katenyi amesema hospitali ya Kabanga inatarajia kuanza ujenzi wa Maabara kubwa ya kisasa ili kuboresha utoaji wa huduma kwa wagonjwa na wanafunzi wanaofika pale kwa ajili ya kujifunza kutoka maeneo mbalimbali ndani na nje ya nchi.
“Leo kuna baadhi mmepata vyeti vya watumishi bora wa mwaka 2025 lakini tunatarajia kuanza ujenzi wa Maabara kubwa ya kisasa kwa ajili ya kuongeza ubora wa utendaji kazi na kutoa huduma bora kwa wagonjwa na wale wote wanaokuja kujifunza hospitalini kwetu” Amesema Dkt. Kitenyi.

Katika hatua nyingine Dkt. Kitenyi amemalizia kwa kusema Askofu Joseph Roman Mlola,ambaye ni Askofu wa jimbo katoriki Kigoma, pia mlezi na mmiliki wa wa hospitali hiyo anatambua uwepo wa watumishi hao kwa kuambatanisha ujumbe wa salamu za pongezi.
“Muda mfupi nimezungumza na Baba Askofu anatambua uwepo wenu hivyo anawasalimia na ametuma ujumbe wa pongezi kutoka jimboni kwa hiyo endeleeni kupongezana kwa kumshuru Mungu kwa kumaliza mwaka tukiwa wazima wa afya”Amesema Dkt. Kitenyi.

Hospitali ya Kabanga iliyo chini ya kanisa Katoliki jimbo la Kigoma ilipata usajili kwa mara ya kwanza kama hospitali binafsi mwaka 1997 na kupewa hadhi ya kuwa hospitali ya rufaa mwaka 2010 chini ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutoa huduma kwa wananchi zaidi ya million 2.3 wa Mkoa wa kigoma na maeneo mengine nchini.