Buha FM Radio
Buha FM Radio
December 19, 2025, 1:58 pm

Wananchi wa Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma wameshukuru huduma za hospitali ya rufaa Kabanga kwa kutoa huduma za vipimo na matibabu bure ikiwa ni wiki ya afya Kabanga iliyoambatana na kauli mbiu ya “Tuungane kutokomeza magonjwa yasiyoambukizwa” iliyofanyika katika viwanja vya kituo cha afya Kiganamo katika Halmashauri ya Mji Kasulu.
Na; Sharifat Shinji
Hospitali ya Rufaa Kabanga katika Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma imeendelea kutoa huduma za vipimo bure kwa wananchi wa Wilaya hiyo ikiwa ni kampeni ya wiki ya afya Kabanga iliyofanyika katika viwanja vya kituo cha afya Kiganamo.
Akizungumza Dkt. Ephraim Kilale ambaye ni mtaalamu wa magonjwa ya macho ameeleza zoezi hilo namna linavyo endelea na kueleza huduma zinazotolewa kuwa ni magonjwa yasiyoambukizwa ikiwemo ugonjwa wa Meno, Presha pamoja na kuwaona madakitari Bingwa wa Hospitali ya Kabanga.

Aidha kwa Upande wake Neema Mwaipopo ambaye ni Afisa mahusiano ya Umma katika Hospitali Kabanga amesema mwitikio wa wananchi katika Wilaya Kasulu ikiwa ni wasitani ya zaidi ya watu 100 kwa siku huku wakiahidi kuendelea kutoa kutoa huduma kwa kuwafikia wananchi katika kata zao.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Kigoma Agripina Buyogela ambaye amehudhuria vipimo katika eneo hilo amepongeza serikali kwa jitihada za kuwaletea wananchi huduma bure huku akitoa wito kwa wananwake kujitokeza kupima magonjwa mbalimbali yanayowasumbua.

Nao baadhi ya wananchi waliojitokza kufanya vipimo wameishukuru hospitali ya kabanga huku wakitoa wito wakuwa na mwendelezo wa huduma hii zaidi ya mara moja kwa Mwaka.

Hospitali ya Rufaa Kabanga huwa inaandaa kampeni ya kutoa huduma bure kila mwaka kwa lengo la kurudisha kwa jamii ikiwa mwaka 2025 kampeni iliyotumika ni wiki ya afya Kabanga ikiambatana na kauli mbiu isemayo “Tuungane kutokomeza magonjwa yasiyoambukizwa”