Buha FM Radio
Buha FM Radio
December 7, 2025, 12:20 pm

Maafisa usafirishaji maalufu Bodaboda kutoka Wilaya mbalimbali mkoani Kigoma wapinga maandamano yaliyopangwa kufanyika Desemba 9, Serikali wilayani Kasulu yatia neno la msisistizo wa kutojihusisha na maandamano hayo.
Na; Sharifat Shinji
Maafisa Usafirishaji wa abiri malufu Bodaboda mkoani Kigoma wamesema hawatoshiriki Maadamano yaliyopangwa kufanyika Desemba 9 mwaka huu na kusema watakuwa mabalozi wa kuzuia vitendo vya uvunjifu wa amani katika Mkoa wa Kigoma na taifa kwa ujumla.
Wakizungumumza katika kikao cha pamoja na cha Maafiasa hao kutoka Wilaya mbalimbali za Mkoa wa Kigoma kilichofanyika katika Halmashauri ya Mji Kasulu akiwemo Makamo Mwenyeiti wilaya ya Kasulu Hamad Kilugu na Mwenyekiti bodaboda Wilaya ya Buhighwe Zaeli Livingstone wamesema watahimiza amani na kutojihusisha na maandamano ya Desemba 9.
Aidha Jeff Mkando ambaye ni Afisa habari wa bodaboda na bajaji mkoa wa Kigoma amepiga marufuku kwa maafisa wote mkoani humo na kuelekeza viongozi kuanzia ngazi za kata hadi Mkoa wanasimamia zoezi la kutoshiriki maandamano hayo.
Kwa upande wake mwakilishi wa mgeni rasmi wa mkutano huo Adriano Mihale Afisa Mtendaji Kata ya Asante Nyerere na Kaimu Afisa Tarafa Heruchini ambaye alikuwa akimwakilisha Mkuu wa Wilaya Mhe. Kanal Isack Mwakisu, amesema ofisi ya mkuu wa Wilaya imesisiti vitendo vya vurugu za maandamano wasijihusishe kwa namna yoyote kwani vitendo hivyo vina madhara makubwa kama yaliyotokea Oktoba 29 mwaka huu.

Kikao hicho kilikuwa na ajenda mbalimbali ikiwemo kuwasilisha changamoto zinazowakabili hasa kuelekea mwisho wa mwaka ambapo huwa wanakutana na usumbufu wa vyombo vya usalama ambapo wameiomba serikali kuzipatia ufumbuzi changamoto hizo.