Buha FM Radio
Buha FM Radio
December 3, 2025, 10:08 pm

Wananchi wa kata ya Makere waomba kujengewa miundombinu ya madaraja katika Kata mbalimbali Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu ili kuondoa ajari za watoto wa shule hasa katika kipindi cha mvua.
Na; Saharifa Shinji
Baadhi ya wakazi wa Kata ya Makere katika Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma wameiomba serikali ya wilaya hiyo kuwatekelezea ujenzi wa daraja kwa kuweka kalavati katika kivuko cha barabara ya kitongoji cha Gwanguge kuelekea shule ya msingi Tulieni.
Wameyasema hayo wakati wakizungumza na Buha FM Radio katika shule ya msingi Tulieni na Kusema kivuko hicho husababisha maafa kwa watoto wanaotumia njia hiyo kwenda shuleni hasa katika kipindi cha mvua.
Aidha Mwenyekiti wa serikali ya Kijiji cha Makere Daniel Bakunda amesema tayari changamoto hiyo ipo kwenye mpango wa kutekelezwa kwa kuweke Karavati huku wakiwa tayari wamejenga baadhi ya vivuko kwa ajili ya kunusuru uhai wa watoto wanaotumia barabara hizo.
Mwenyekiti amasisitiza kwa kuwaomba wazazi wawapeleke watoto shule kwani tayari miundombinu ya barabara inaendelea kutekelezwa ili kuwarahishia watoto kufika shule salama bila changamoto yotote huku baadhi ya changamoto kubwa za madaraja akiwa amezifikisha kwa Mkuu wa Wilaya kwa ajili ya utatuzi zaidi.
