Buha FM Radio
Buha FM Radio
November 26, 2025, 12:40 am

Wadau wa maendeleo wa miradi ya World VisionTanzania katika Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu wameombwa kuitunza miradi inayotekelezwa na shirika hilo ili ije kusaidia vizazi vijavyo.
Na; Ramadhan Zaidy
Shirika la maendeleo la World Vision Tanzania linalotekeleza miradi katika Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma limewataka Wanufaika wa miradi hiyo kuitunza na kuilinada miradi yote inayojengwa na kuendelezwa mkoani humo ili iweze kunufaika kwa muda mrefu.
Wito huo umetolewa na Meneja wa Western Cluster Jacklin Kaihura wakati wa kikao kilichowakutanisha wadau wa miradi inayosimamiwa na kuendeshwa na Shirika hilo, wilayani humo na kusema kutunzwa na kuendelezwa kwa miradi hiyo kutasaidia wananchi wengi na kunufaika kizazi cha badae.

Kwa upande wake Mratibu wa Miradi ya Buhoro na Nyakitoto Esther Mshendwa ameeleza shughuli zilizotekelezwa na shirika hilo na ikiwa ni pamoja na Afya na lishe, maji na Utunzaji wa mazingira, elimu, jinsia ulinzi na haki za mtoto katika jamii.
Aidha Mratibu Bi. Mshendwa ameongeza kuwa shirika hilo limetoa mafunzo kwa wazazi juu ya ulinzi wa mtoto na mwanamke pamoja na kutoa mikopo kwa ajili ya kujiinua kiuchumi kwa wanufaika wa mradi huo.
Naye Mgeni rasmi katika Kikao hicho ambaye ni Mkurungenzi wa Halmashari ya Wilaya ya Kasulu, Francis Kafuku amelipongeza shirika la world Vision kwa kuendeleza miradi mbalimbali wilayani Kasulu na kuboresha maisha ya wananchi.

Katika hatua nyingine baadhi ya wananchi na wanufaika wa miradi hiyo wamesema katika kipindi chote cha utekelazi wa miradi, shirika hilo limewasaidi kujiinua kiuchumi pamoja na kupata elimu za ujasiliamali.
Shirika la World Vision Tanzania ni shirika la kikisriso lisilo la kiserikali lenye kufanya shughuli mbalimbali ndani na nje ya nchi likiwa limejikita katika kuinua jamii katika sekta mbalimbali ili kufanya istawi kwa kulenga zaidi watoto, Wakiwemo watoto wanaishi mazingira magumu.