Buha FM Radio
Buha FM Radio
October 17, 2025, 5:40 pm

“NCCR Mageuzi hatuko tayari kuona uchaguzi unaingiliwa au kuvurugwa na wahuni kwa mwavuli wa Maandano kwa sababu hii chama kinawaagiza wagombea wake, viongozi, wanachama, mashabiki na marafiki zetu kwenda kupiga kura” Amesema ndg Faustine.
Na; Irene Charles
Mkuu wa idara ya sheria, katiba na haki za binadamu kupitia chama cha NCCR mageuzi Ndg. Faustine Sungura amewaomba wanachama pamoja na wananchi kutofanya maandamano badala yake wajitokeze kwa wingi kushiriki uchaguzi mkuu utakaofanyika oktoba 29 mwaka huu.
Amebainisha hayo oktoba 16,2025 wakati akizungumza na waaandishi wa habari katika ukumbi wa upendo uliopo halmashauri mji Kasulu mkoani Kigoma amesema baadhi ya watu wanaojipanga na maandamano tarehe 29 wanafanya hivyo kwaajili ya kuleta taaruki na kuzuia uchaguzi.
Aidha ndg. Faustine amewataadharisha wananchi kutofanyanya maandamano yatakayo leta uhalibifu wa mali za umma huku akiwaomba viongozi walipo madarakani kukemea na kuwakamata watu wanaohamasisha maandamano hayo.
Katika hatua nyingine Ndg. Faustine Sungura amesema serikali inapaswa kuwatazama na kuwapa kipaumbele watu wenye ulemavu katika nafasi za uongozi kupitia uchaguzi mkuu oktoba 29,2025.
“Kwa sababu Chama Cha Mapinduzi (CCM) na NCCR mageuzi ilani yetu ya Uchaguzi, inayowahusu watu walio katika makundi maalumu, hususani wenye wenye ulemavu” Amesema Ndg Sungura.

Katika wiki kadhaa za hivi karibuni kumekuwa na baadhi ya vijana wanaohamasisha maandamano kupitia mitandao ya kijamii ifikapo Octoba 29 mwaka huu siku ya uchaguzi kwa lengo la kuzuia uchaguzi huo.