Buha FM Radio
Buha FM Radio
September 20, 2025, 1:50 am

“Kukamilika kwa daraja hili tunapaswa kuwapongeviongozi wetu wa kipindi cha utekelezaji mradi huu mbunge wetu Ndalichako kwa kweli kwenye hili tunakukumbuka sana na ninaomba tumpigie makofi kwa jitihada ulizozifanya unasitahili pongezi kwa kushirikiana na viongozi hadi kukamilika kwa daraja hili” Amesema Ussi kiongozi wa mbio za mwenge 2025.
Na; Sharifat Shinji
Baadhi ya wananchi waliojitokeza katika uzinduzi wa Daraja la Mawe Nyatale katika Halmashauri ya Mji Kasulu mkoani Kigoma wameshukuru viongozi wa serikali kwa jitihada walizofanya kuhakikisha daraja hilo linakamilika katika eneo hilo.
Shukurani hizo wamezitoa wakati wa zoezi la uzinduzi na Uwekaji wa Jiwe Msingi la uzinduzi wa daraja hilo na kueleza jinsi ambavyo walikuwa wakipitia adha kubwa hasa katika kipindi cha mvua ambapo watoto wengi walishindwa kuhudhuria masomo na wengine kupoteza maisha kwa kusombwa na maji.

Aidha kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa Ndg. Ismail Ussi amesema mradi huo umetekelezwa kwa ubora wa juu na kuwapongeza viongozi waliosimamia mradi huo huku akimtaja Joyce Ndalichako mbunge aliyesimamia kikamilifu mradi huo.

Katika Hatua nyingine Mkuu wa Wilaya ya Kasulu Mhe. Kanali Isack Mwakisu ameeleza namna daraja hilo lilivyositisha shughuli za usafirishaji kipindi cha mvua na kukatisha ndoto za wanafunzi wengi waliokosa masomo na wengine kupoteza maisha kutokana na maji kujaa katika eneo hilo.
Awali akisoma taarifa kwa Kiongozi wa mbio za Mwenge Kitaifa Mhandisi Sezia Maheda Meneja wa TARURA Wilaya ya Kasulu amesema Mradi huo umetekelezwa na serikali kwa kutumia fedha kutoka Bank ya Dunia ya miradi ya kuondoa vikwazo katika jamii.
Kwa mjibu wa Mhandisi Maheda Meneja wa TARURA Wilaya ya Kasulu Daraja limegharimu zaidi ya Milioni 100 likiwa na urefu wa mita 28 ambapo ulianza kutekelezwa mwezi juni 2024 na limemeanza kutumika Septemba mwaka huu.
