Buha FM Radio
Buha FM Radio
September 17, 2025, 6:19 pm

Leo Septemba 17, 2025 Mkuu wa Wilaya ya Kasulu Mhe. Kanal Isack Mwakisu amepokea mwenge wa Uhuru 2025 na wakimbiza Mwenge kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Kibondo Mhe. Kanal Aggrey Magwaza huku akiwakaribisha wote waliojitokeza katika makabidhiano hayo.
Na; Sharifat Shinji
Mkuu wa Wilaya ya Kasulu Mhe. Kanal Isack Mwakisu amesema Jumla ya Billion 2.75 imetumika Katika utekelezeji wa Miradi 14 katika Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma ambayo itapitiwa, kukaguliwa na kuwekewa jiwe la Msingi pamoja na kuzinduliwa na Mwenge wa Uhuru 2025.
Amesema hayo Leo wakati makabidhiano ya Mwenge wa Uhuru 2025 katika viwanja vya shule ya Msingi Mvugwe na kusema mwenge utakimbizwa Halmashauri mbili za wilaya ya Kasulu ambazo ni Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu na Halmashauri ya mji Kasulu.
Aidha Mwakisu amesema Wilaya ya Kasulu imejipanga kuhamasisha uchaguzi mkuu kupitia mikutano mbalimbali pamoja na kushirikisha vyombo vya habari vilivyopo katika Wilaya ya Kasulu pamoja na tarifa kupitia kauli mbiu ya mbio za mwenge inavyosema “jitokeze kushiriki Uchaguzi Mkuu kwa Amani na Utulivu”.

Mwenge wa uhuru mwaka 2025 umekabidhwa Leo Septemba 17 kwa Mkuu wa Wilaya ya Kasulu Mhe. Kanal Isack Mwakisu ukitokea katika Wilaya ya Kibondo na utakimbizwa Wilaya ya Kasulu kwa Siku mbili ambapo Septemba 17 utakimbizwa Halmashauli ya wilaya ya Kasulu na Septemba 18 utakimbizwa katika Halmashauri ya Mji Kasulu na kukabidhiwa wilayani Buhigwe Mkoani kigoma Septemba 19.
