Buha FM Radio
Buha FM Radio
September 10, 2025, 10:04 pm

“Watanzania angaliyeni mataifa mengine nilipata nafasi ya kwenda Sudan kwenye ukaguzi unaona namna wananchi wanavyohangaika hadi watoto wadogo wanajuwa namna ya kuomba msaada pia nilienda Congo na kwenyewe niliona namna watu wanavyoteseka kuitafta amani nikawa nawaza Watanzania wangekuwa wanapata nafasi ya kutoka wangejifunza namna Amani ilivyo na umhimu katika jamii” Amesema IGP. Siro.
Na; Sharifat Shinji
Kuelekea uchaguzi mkuu utakaofanyika Octoba 29, 2025 waumini wa Dini mbalimbali katika Halmashauri ya Mji Kasulu Mkoani Kigoma wamekusanyika na kuandaa kongamano la ibaada ya kuombea uchaguzi mkuu pamoja na kuwaombea wagombea katika nafasi mbalimbali za uongozi nchini.
Kongamano hilo la ibada limefanyika katika Ukumbi wa Bwalo la Chuo cha Walimu Kasulu TTC Septemba 09 na kuhudhuliwa na mgeni rasimi ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Kigoma IGP Mstafu, Mhe. Balozi Saimon Siro pamoja na Wakurugenzi wa Wilaya ya Kasulu na Viongozi mbalimbali wa dini.
Sheikh Nasibu Rajabu ambaye ni Sheikh wa Mkoa Shia (TIC) ameeleza namna amani ambavyo inaweza kuwaweka pamoja Watanzania huku akihubiri maneno ya Mtume Mohammad (S.A. W) juu amani kwa wananchi.

Kupitia kongamano hilo IGP Siro ambaye ni mgeni rasmi amesema ili Taifa liendelee kuwa salama ni lazima viongozi wa dini washikamane kwa kuliombea Taifa na kulinda amani iliyopo katika Taifa la Tanzania na kusisitiza umuhimu wa viongozo wa dini katika Jamii.

Aidha IGP ameongeza kwa kuwaomba viongozi wa dini kuhubiri dini kwa kuzingatia mipaka yake pamoja na kuzingatia maadili ya Watanzani ambayo yataendelea kudumisha amani katika Taifa la Tanzania huku akiwataka wazazi kuhusika katika maelezi ya watoto katika familia ili kutengeneza jamii iliyo bora.

Katika hatua nyingine Kamanda Siro amesema katika swala la uchaguzi serikali imejipanga kusimamia kikamilifu huku akiwasisitiza wananchi kusikiliza kampeni za wagombea na kuwaomba kushiriki siku ya kupiga kura huku akitaja maendeleo yaliyofanyika katika Mkoa wa kigoma chini ya Dkt. Samia Suluhu Suluhu Hassan.

Akimalizia Askofu Josephat Kilibaze Mwenyekiti wa Kamati Maridhiano Tanzania amewakumbusha viongozi wa dini kuhakikisha wanayachukuwa yote yaliyosemwa na Mgeni rasmi juu ya mipaka na kuyazingatia yote waliyoyahubiri kwenye Kongamano hilo ili kulinda amani kuelekea uchaguzi mkuu mwaka huu.
Kongamano hilo limefanyika mahususi kwa ajili ya kuombea uchaguzi mkuu mwaka 2025 utakaofanyika Octoba 29 pamoja na kuwaombea nafasi ya Udiwani, Ubunge na Urais katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Taifa kwa ujumula ili kudumisha amani ya Watanzania.
