Buha FM Radio
Buha FM Radio
September 8, 2025, 1:01 pm

Mkuu wa Wilaya ya Kasulu Mhe. Kanal Isack Mwakisu amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na mgombea Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM atafanya kampeni katika Wilaya ya Kasulu Septemba 13 mwaka huu.
Na; Sharifat Shinji
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mgombea Urais kupitia cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwasili wilayani Kasulu mnamo Septemba 13 mwaka huu kwa ajili ya kunadi sera zake za kampeni za uchaguzi mkuu utakaofanyika Octoba 29 mwaka huu.
Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Wilaya ya Kasulu Mhe. Kanal Isack Mwakizu wakati wa ufunguzi wa Bonanza la kuukaribisha mwenge wa Uhuru mwaka 2025 lililofanyika October 6 katika uwanja wa Kiganamo katika halmashauri ya Mji Kasulu.

Aidha Mwakisu amewasisitiza wananchi kushiriki kampeni kwa amani na utulivu pamoja na kujitokeza kushiriki uchaguzi mkuu kwa amani na utulivu siku ya tarehe 29 mwezi octoba mwaka huu.
Sauti ya Mkuu wa Wilaya ya Kasulu Mhe. Mwakisu akiwaomba wananchi kujitokeza kusiriki uchaguzi mkuu Octoba 29 mwaka huu.
Katika hatua nyingine akizungumza Rebeka Eza ambaye ni Afisa Mipango Halmashauri ya Mji Kasulu ambaye ni mdau wa bonanza amewasisitiza wananchi wa Wilaya Kasulu kujitokeza kushiriki uchaguzi mkuu wa Octoba 29 mwaka huu.
Hata hivyo Bonanza hilo limeandaliwa na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kasulu kwa ajili ya mapokezi ya mbio za mwenge wa Uhuru mwaka 2025 likiwa na kauli mbio isemayo “jitokeze kushiriki uchaguzi mkuu mwaka 2025 kwa amani na Utulivu”.