Buha FM Radio
Buha FM Radio
August 27, 2025, 9:19 pm

Kwa mama mwenye mtoto anatakiwa baada ya kumsafisha mtoto kuhakikisha ananawa mikono vizuri kumkinga mtoto, hata hivyo viongozi wa taasisi, masoko wanatakiwa kuweka maji tiririka amesema mratibu Mwita.
Na Irene Charles
Wananchi Kasulu watakiwa kuchukua taadhari ili kuepukana na tatizo la kuhara na kutapika kwa kunawa mikono kwa maji tiririka na sabuni , matumizi sahihi ya choo kwa kuwa safi mda wote, kuepuka kusalimiana au kupongezana kwa njia ya mkono.

Hayo yamebainishwa na afisa afya wa halmashauri ya Mji Kasulu Ndg. Malimi Temi kupitia kipindi cha shangwe la asubuhi amesema mwananchi atakaebaini dalili za kuhara na kutapika anatakiwa kufika kituo cha afya ili kupata huduma mapema.
Afisa Malimi amesema kwa sasa wamepata dawa ya vidonge kwaajili ya kutibu maji kwa gazi ya kaya, wahudumu ngazi ya jamii watapita kutoa dawa hiyo kwa wananchi ambao wamepatwa na changamoto hiyo huku wakiendelea kuangalia vyanzo vya maji.
Kwa upande wake mratibu wa afya kwa umma Ndg. Mwita Range amesema usafi sehemu ya kuandalia chakula pamoja na vyombo unaitajika kwa kiwago cha juu na kulinda maji na vyanzo vyake ili kuepusha kupata vimelea.
Kwa mama mwenye mtoto anatakiwa baada ya kumsafisha mtoto kuhakikisha ananawa mikono vizuri kumkinga mtoto, hata hivyo viongozi wa taasisi, masoko wanatakiwa kuweka maji tiririka amesema mratibu Mwita.

Aidha afisa lishe Ndg. John Sabatele amesema kuhara na kutapika kunaweza kusababisha upungufu wa lishe mwilini kwa kukosa virutubisho na kupata utapiamlo , muda mwingine kupelekea mpaka kifo.
Mpaka sasa watu wawili wamepoteza maisha kutokana na ungonjwa huu ambao haujajulikana mmoja akitoka kata ya Kigondo mtaa wa Nyarumanga na wapili kutoka kata ya Murusi mtaa wa Hwazi