Buha FM Radio

Ndalichako achukuwa fomu tena kulitetea Jimbo la Kasulu Mjini

August 27, 2025, 5:57 pm

Mgombea ubunge jimbo la Kasulu Mjini Prof. Ndalichako akikabidhiwa fomu za ugombea Ubunge Kasulu Mjini 2025. Picha na Sharifat Shinji.

Prof. Joyce Ndalichako asindikizwa na umati wa wanachama kuchukua fomu za kugombea ubunge Jimbo la Kaulu Mjini kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi CCM kwa awamu ya pili 2025-2030 baada ya kumaliza awamu ya kwanza mwaka 2020-2025 na kuahidi mazuri ndani ya jimbo hilo.

Na; Sharifat Shinji

Mgombea Ubunge katika Jimbo la Kasulu Mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM Prof. Joyce Ndalichako amechukua Fomu ya kugombea nafasi hiyo akiwa ameambatana na mgombea Ubunge kutoka Jimbo la Kasulu Vijijini Bw. Edibili Kazala pamoja na wanachama na kuahidi kulitetea Jimbo hilo kwa nguvu zote.

Zoezi hilo la uchukuwaji Fomu limefanyika Agosti 26 katika ofisi ya msimamizi wa uchaguzi jimbo la Kasulu Mjini Bw Azizi katika jengo la Halmashauri ya Mji Kasulu.

Prof. Ndalichako akiwa kwenye maadamano kuelekea ofsi ya Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Kasulu Mjini akiwa ameambatana sambamba na mgombea ubunge jimbo la Kaulu Vijijini Bw. Edibili Kazala. Pischa na Sharifat Shinji.

Aidha baada ya zoezi la kuchukua Fomu hizo Ndalichako alizungumza na umati uliojitokeza kumsindikiza katika zoezi hilo na kuwashukuru kwa kuendelea kumuunga mkono huku akiahidi kushinda nafasi hiyo na kukitetea chama hicho.

Sauti ya Ndalichako akizungumza na wananchi.

Ndalichako meongeza kwa kuwaomba wananchi kujitokeza katika zoezi la kampeni ambazo zinatarajiwa kufunguliwa rasmi kitaifa Agosti 28 ili kusikiliza Sera na kampeni za wagombea huku akiahidi kufanya kampeni za amani bila kutweza utu wa mtu na kwa kuzingatia Demokrasi ya nchi na vyama vingine vya siasa.

Ndalichako akisaini fomu za kugombea nafasi ya ubunge JImbo la Kasulu Mjini katika ofis ya Msimamizi wa Uchaguzi jimbo la Kasulu.
Sauti ya Ndalichako akizungumza na wananchi.

Katika hatua nyingine mgombea Ubunge katika jimbo la Kasulu Vijijini Ndg. Edibili Kazala ameahidi kuendeleza ushirikiano na jimbo la Kasulu Mjini ili kuleta maendeleo ya pamoja na kuwashukuru wananchi wote wa jimbo lake waliojitokeza katika zoezi hilo na kusema atawalipa Utu.

Mgombea ubunge jimbo la Kasulu Vijijini kulia na Kushoto ni Mgombea Ubunge jimbo la Kaulu Mjini.Picha na Sharifat Shinji.
Sauti ya Edibili Kazala mgombea Ubunge Jimbo la Kasulu Vijijini.

Naye mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM wilayani Kasulu Ndg. Mbelwa Abdallah amewashukuru wanachama wa Chama hicho kwa kuendelea kuunga mkono huku akiwaomba wagombea watakapo pata ridhaa ya kuchaguliwa wakawatumikie wananchi bila kubagua wala kupendelea mtu yeyote.

Sauti ya mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM wilayani Kasulu Ndg. Mbelwa Abdallah.

Kwa mujibu wa mwenyekiti Mbelwa kampeni Wilaya ya kasulu zitazinduliwa rasmi Agost 31 mwaka huu huku tarehe 28 na 29 ikiwa ni mipango ya uzinduzi wa kampeni hizo kwa viongozi wa majimbo nakata kukaa vikao vya ndani.

Mgombea ubunge Jimbo la Kasulu Mjini Prof. Ndalichako (katikati) akiwa ameongozana na Viongozi wa Chama Wilaya ya Kasulu kuelekea kuchukua Fomu za kugombea Ubunge 2025-2030. Picha na Sharifat Shinji