Buha FM Radio

Raia wa kigeni chanzo vitendo vya wizi, uhalifu, mauaji Kigoma

August 9, 2025, 11:36 am

Nuhu Fyelo mkazi na Mfanyabiashara kutoka Halimashauri ya Mji Kasulu. Picha na Emily Adam.

Wamesema licha ya raia hao kuwasaidia katika shughuli za mashambani lakini kuna baadhi yao ambao sio waaminifu wamekuwa wakitumia nafasi hiyo kufanya vitendo vya kiuharifu hasa wizi na ujambazi kwa kutumia silaha.

Na Emily Adam

Wananchi na wafanyabiashara Halmashauri ya mji Kasulu mkoani Kigoma wameiomba serikali wilayani humo kuwaondoa raia wa kigeni waliongia kinyume cha sheria ili kupunguza kasi ya vitendo vya wizi, uharibifu pamoja na ujambazi kwenye maeneo ya wilaya hiyo.

Wamesema hayo wakati wakiongea na Buha FM Radio juu uwepo wa wimbi kubwa wa raia wa nchi za kigeni hasa kutoka Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ambao huingia kuishi Tanzania bila kuwa na vibali vinavyo watambulisha jambo linalokuwa likileta hofu kwa usalama wa watanzania na mali zao.

Nuhu Fyelo na Josefu Haruni ni baadhi ya wakazi na wafanyabiashara kutoka Halimashauri ya  Mji Kasulu wamesema kuwa licha ya raia hao kuwasaidia katika shughuli za mashambani lakini kuna baadhi yao ambao sio waaminifu wamekuwa wakitumia nafasi hiyo kufanya vitendo vya kiuharifu hasa wizi na ujambazi kwa kutumia silaha.

Sauti ya Wananchi

Kwa upande wake mkaguzi msaidizi wa Jeshi la polisi  wilayani kasulu AINSP Willi Lupa amesema kuwa jukumu la kuimarisha ulinzi, usalama pamoja na kuzuia na kutokemeza vitendo vya uhalifu na uvunjifu wa amani ni jukumu la kila mwananchi huku akiwataka wakazi wa wilaya hiyo kuendelea kutoa ushirikiano kwa Jeshi la polisi ili kuhakikisha wanaimarisha usalama muda wote.

Sauti ya AINSP Willi Lupa

Vitendo vya wizi, uharifu na mauwaji  katika baadhi ya maeneo ya wilaya ya Kasulu mkoai Kigoma vimekuwa vikitokea huku wakazi wa wilaya hiyo wakidai hutekelezwa kutokana na kuwepo kwa mwingiliano wa raia wa kigeni ambapo wengi wao huingia nchini kwa kutumia mipaka iliyopo katika wilaya za buhigwe,kibondo na kakonko.