Buha FM Radio

Madereva, watembea kwa miguu watakiwa kufuata sheria barabarani

July 1, 2025, 11:22 am

Mrakibu na Mkuu wa Polisi usalama barabarani wilaya ya Kasulu Patrick Damas. Picha na Irene Lucas

Mwezi Juni kumetokea ajali katika sehemu mbalimbali kwa mkoa wa Mbeya watu 28 walifariki lakini mkoa wa Kilimanjaro watu 38 wamefariki huku mkoa wa Sumbawanga watu 6 wamefariki na mamia kati yao wakiendelea na matibabu kutokana na majeraha yaliyotokana na ajali hizo.

Na Irene Lucas

Mrakibu na Mkuu wa Polisi usalama barabarani wilayani Kasulu mkoani Kigoma Patrick Damas Amesema kwa asilimia kubwa makosa ya kibinadamu na kutofuata sheria za usalama barabarani yamekuwa yakisababisha ajali nyingi katika wilaya hiyo.

Amesema hayo wakati akizungumza na Buha FM Radio ofisini kwake na kusema ili kukabiliana na makosa hayo wameendelea kukutana na madereva pamoja na abiria kwa lengo la kuwapa elimu ya kutosha juu ya matumizi sahihi ya barabara.

Sauti ya Mrakibu Patrick Damas.

Aidha Mrakibu Patrick amesema utoaji wa elimu juu ya matumizi sahihi ya barabara imegawanjika katika makundi mbalimbali ambayo ni kwa madereva, abiria, watembea kwa miguu na maafisa usafilishaji maarufu kama Bodaboda.

Sauti ya Mrakibu Patrick Damas.

Sanjali na hayo Mrakibu Patrick ametoa wito kwa madereva pamoja na watumiaji wengine wa barabara kufuata sheria za usalama barabani na pale wanapoona matuko ya ajali au  uvunjifu wa sheria watoe taarifa katika kituo cha polisi.

Sauti ya Mrakibu Patrick Damas.

Nao baadhi ya wananchi ambao pia ni watumiaji wa barabara wamesema madereva wanatakiwa kuwa makini wakati wakiwa wanaendesha pamoja na uwekwaji wa matuta barabarani ili kupunguza ajali zinazojitokeza kutokana na mwendokasi.

Sauti ya Mwananchi ambae pia ni mtumiaji wa barabara.

Ikumbukwe ndani ya mwezi Juni kumetokea ajali katika sehemu mbalimbali kwa mkoa wa Mbeya watu 28 walifariki lakini mkoa wa Kilimanjaro watu 38 wamefariki huku mkoa wa Sumbawanga watu 6 wamefariki na mamia kati yao wakiendelea na matibabu kutokana na majeraha yaliyotokana na ajali hizo.