Buha FM Radio

Madereva wa magari waonywa kuegesha vibaya Mnadani

June 14, 2025, 10:56 am

Baadhi ya magari yaliyoegeshwa barabarani eneo la soko la Mnadani. picha na Emil Adam

Wito huo umetolewa na mkaguzi wa magari kutoka Jeshi la polisi wilayani Kasulu Koplo Fadhili Ndege wakati akiongea na Buha FM Radio akiwa sokoni hapo juu ya namna madereva wa magari wanavyopaki wakati wanapakia mizigo kwa ajili ya kuisafirisha sehemu mbalimbali.

Na Emil Adam

Madareva wa magari makubwa yanayobeba mizigo ya bidhaa za mazao katika soko la mazao la Mnadani lililopo katika halmashauri ya Mji Kasulu mkoani Kigoma wametakiwa kuepuka kupaki magari hayo barabarani wakati wa kupakia mizigo ili kuruhusu watumiaji wengine kupita katika barabara hiyo kwa urahisi pamoja na kuepuka msongamano na ajali zisizo za lazima.

Wito huo umetolewa na Mkaguzi wa magari kutoka Jeshi la polisi Wilaya ya Kasulu Koplo Fadhili Ndege wakati akiongea na Buha FM Radio akiwa sokoni hapo juu ya namna madereva wa magari makubwa wanavyopaki wakati wanapakia mizigo kwa ajili ya kuisafirisha sehemu mbalimbali.

Koplo Fadhili Ndege ameongeza kuwa madereva hao wamekuwa wakipaki magari yao barabarani huku wakikwepa kuyapaki eneo lilitengwa kwa ajili ya maegesho ya magari jambo linalo kuwa likileta usumbufu wa kuzuia barabara na kusababisha changamoto kwa watumiaji wengine hususani wale wenye magari madogo, pikipiki, baiskeli pamoja na watembea kwa miguu.

Sauti ya Koplo Fadhili Ndege.

Aidha, Koplo Ndege amewaasa madereva wote kwa ujumla kuzingatia sheria na kanuni za matumizi sahihi ya barabara na kuonya kuwa hatua kali zitachuliwa kwa wale wote watakaokaidi agizo hilo.