Buha FM Radio
Buha FM Radio
May 30, 2025, 1:24 am

Mwenyekiti wa maafisa usafirishaji katika Halmashauri ya Mji Kasulu wameonywa juu ya matumizi ya sahihi ya barabara ili kuepuka ajali ambazo zinaweza kujitokeza kutokana na uvunjifu wa sheria za barabara.
Na: Irene Charles
Maafisa usafirishaji abilia kwa njia ya Pikipiki wameshauriwa kufuata sheria za barabarani ili kuepukana na ajali zinazotokea kutokana na ukosefu wa elimu ya kutosha juu ya matumizi sahihi ya Barabara na vyombo vya moto.
Ushauri huo umetolewa leo na mwenyekiti wa umoja wa maafisa usafirishaji UMWAPIKI katika Halmashuari ya Mji Kasulu mkoani Kigoma Ndg. Daud Mathias wakati akizungumza na Buha FM radio katika kipindi cha ‘Darasa nje ya shule’ na kusema vifo vingi vinatokea kwa sababu ya baadhi ya maasifa hao kutofata sheria na taratibu zilizowekwa ili kulinda usalama wao.
Aidha mwenyekiti Daud amewataka a madereva wote katika Halmashauri ya Mji Kasulu kufata sheria na kuchukua tahadhari kipindi wanapokuwa barabarani ili kujiepusha na ajali ambazo zinaepukika pamoja na kuwasihi kujiunga katika vituo vya usafirishaji ili kupata sifa ya kusajiliwa katika umoja huo.
Katika hatua nyingine Mwenyekiti Daud amesema madereva wamewekewa utaratibu wa kufuata katika zoezi la ubebaji wa abilia pale anapofika katika vituo vyao kwa awamu ili kuepusha vurugu ya kukimbilia abilia jambo linaloweza kusababisha ajali na usumbufu kwa abilia anayehitaji huduma hiyo.
Kwa upande wake katibu wa mkoa na mhasibu wa umoja huo Ndg. Khalifan Said amesema abilia au afisa usafirisha akifika kituo cha mabasi muda wa usiku kama safari sio ya lazima ni bora zaidi kubaki na kusubiri mpaka asubuhi kwa ajili ya usalama wake na mali zake.
Baadhi ya Maafisa usafirishaji wamehizana na kushauriana kufuata sheria za usalama barabarani pamoja na kuzingatia vitu wanavyopaswa kuwavitumia wanapokuwa barabarani wakitaja uvaaji wa kofia ngumu pamoja na kuweka Sidemirror ili kuwasaidia kuepukana na ajali ambazo zinaweza kuepukika.
Mwaka 2024, ajali zinazohusisha pikipiki maarufu kama bodaboda, ziliendelea kuwa changamoto kubwa ya usalama barabarani nchini Tanzania, ripoti zinaonyesha kuwa kati ya mwaka 2022 hadi 2024, jumla ya wananchi 1,113 walipoteza maisha kutokana na ajali za bodaboda. Katika idadi hii, madereva walikuwa 759, abiria 283, na watembea kwa miguu 71

Pichani baadhi ya maafisa Usafirishaji Katika Halmashauri ya Mji Kasulu wakiwa katika Ofisi yao wakiendelea na zoezi la Kujisajili katika Umoja wao. Picha na Mbaraka Shaban.