Buha FM Radio

Mpango wa m mama unavyosaidia wajawazito na watoto

May 2, 2025, 2:22 pm

Picha ni muuguzi mkuu na mratiba wa mpango wa m mama Halmashauli ya mji Kasulu Dkt. Agustine Mjuni Kaloli akizungumza na mwandishi wa habari Buha FM Radio. Picha na Emily Adam

“Jumla ya madereva 20 ndio waliohitajika, 9 wamesajiliwa na hulipwa Tshs 1,500/= kwa kilomita 1 na hulipwa kwenda na kurudi” Amesema Dkt. Agustine Mjuni Kaloli.

Na Sharifat Shinji

Muuguzi Mkuu katika Halmashauri ya Mji Kasulu ameeleza jinsi mpango wa m mama unavyowasaidia wajawazito na wanawake wenye watoto wachanga kupata huduma za kiafya katika vituo mbalimbali katika Halmashauri ya Mji wa Kasulu.

Dkt. Karoli amesema mpaka Sasa mpango wa m mama umenufaisha jumla ya madereva wa magari binafsi 9 wanaosafirisha wanawake wajawazito kutoka kituo kimoja kwenda kingine wanaopewa rufaa.