Buha FM Radio
Buha FM Radio
May 1, 2025, 6:18 pm

Mawakala wa vyama vya siasa wameruhusiwa kuwepo katika vituo vya uandikishaji wakati wote wa zoezi la uboreshaji wa Daftari la kudumu la mpiga kura awamu ya pili katika wilaya ya Kasulu.
Na; Sharifat Shinji
Mawakala wa vyama vya siasa wameruhusiwa kukaa na kushiriki katika vituo vya uandikishaji kwa muda wote katika zoezi la uboreshaji wa Daftari la kudumu la wapiga kura awamu ya pili ili kuhakikisha zoezi hilo linafanyika kwa uwazi na weledi.
Akizungumuza Aprili 29, Afisa Mwandikishaji wa Jimbo la Kasulu vijijini, Emmanuel Ladislaus wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya uboreshaji wa Daftari hilo katika Chuo cha Walimu Kasulu, na kueleza ushiriki wa mawakala hao itasaidia zoezi hilo kufanyika kwa ubora zaidi huku akiwaonya kuingilia majukumu ya maafisa uandikishaji wa zoezi hilo.
Aidha amewataka washiriki wa mafunzo hayo kuhakikisha wanatunza vifaa vyote vitakavyotumika katika Shughuli ya uandikishaji na maelekezo lekezo yatakayotolewa na Afisa wa zoezi la uandikishaji ili kuepuka changamoto ambazo zinaweza kujitokeza wakati zoezi hilo likiendelea.
Kwa upande wao baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo wamesema elimu waliyopewa itawasaidia kufanya kazi hiyo kwa weledi na kuahidi kuwahamasisha wanchi wa Kasulu kushiriki katika zoezi hilo ili washiriki katika zoezi la uchaguzi mkuu mwaka huu.
Zoezi la uandikishaji na uboreshaji wa daftari la kudumu la mpiga kura awamu ya pili linatarajiwa kuanza Mei 1 hadi 7, 2025. Wananchi wote wenye sifa wanahimizwa kujitokeza kwa ajili ya kujiandikisha na kuhakiki taarifa zao za awali kama hazipo sahihi.
