Buha FM Radio

Kasulu utupaji taka maeneo ya kazi bado changamoto

April 30, 2025, 12:22 pm

Picha ni Jalala maeneo ya shughuli za Biashara na makazi ya watu Mtaa wa Shayo katika Halmashauri ya Mji Kasulu. Picha na Ramadhan Zaidy.

Shirika linalojihusisha na utunzaji wa Mazingira katika Halmashauri ya Mji Kasulu (Earth Care Foundation) laeleza namna mabadiliko ya tabianchi yanavyoleta athari katika maeneo ya kazi.

Na; Sharifat Shinji

Wananchi katika Halmashauri ya Mji Kasulu mkoani Kigoma wameombwa kutunza Mazingira ili kuepuka kukabiliana na changamoto ya Mabadiliko ya Tabianchi ambayo yanaweza kuathiri hali ya uzalishaji mali katika maeneo yao ya Kazi.

Akizungumza na Buha Fm Radio leo Msimamizi wa shughuli za Mazingira kutoka Shirika la Earth Care Foundation Bi. Hapines Njile amesema jukumu la kutunza na kulinda mazingira ni la kila mtu kwa sababu linawakabili watu wote na jamii nzima.

Sauti ya Hapines Njile 01

Aidha Njile amesema mabadiliko ya Tabianchi yanathiri katika maeneo mbalimbali ya shughuli za kila siku hivyo wamejitahidi kutoa elimu kwa wananchi Pamoja na kutembelea shule mbalimbali katika Wilaya ya Kasulu ili kuwapa elimu na njia ya kutunza mazingira ikiwemo kupanda miti ili kuzuia na kupunguza madhara yanayoweza kujitokeza katika Jamii.

Sauti ya Hapines Njile 02

Kwa upande wao Kayaya, Diana Deba na Abender Junior ambao ni baadhi ya wananchi katika Halmashauri ya Mji Kasulu wameeleza jinsi wanavyoweza kutunza mazingira na kuiomba  serikali kutilia mkazo katika zoezi la kutunza mazingira ili kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi katika Wilaya ya Kasulu na taifa kwa ujumla.

Sauti za wananchi

Mkutano wa COP29 uliofanyika nchini Azerbaijan mwaka huu ulipitisha na kukubaliana kutoa angalau dola trilioni 1.3 kila mwaka hadi 2035 kwa nchi maskini ili kuzisaidia kupambana na mabadiliko ya tabianch, ambapo kila nchi tajiri itachangia angalau dola bilioni 300 kila mwaka, huku Tanzania ikionekana kukabiliwa na changamoto ya mabadiliko ya tabianchi mahala pa kazi kama alivyobainisha Waziri wa nchi ofisi ya Waziri mkuu, kazi, vijana, ajira na watu wenye ulemavu Mhe. Ridhiwani Kikwete.

Picha ni Msimamizi wa shughuli za Mazingira kutoka Shirika la Earth Care Foundation Bi. Hapines Njile. Picha na Mbaraka Shabani.