Buha FM Radio
Buha FM Radio
April 23, 2025, 1:54 pm

Mkurugenzi mtendaji katika wilaya ya Kasulu Vijijini amewapongeza viongozi hao kwa nafasi waliyochaguliwa.
Na Sungura Jeremiah
Viongozi wa Teule wa Serikali za mitaa katika Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu wamejitokeza katika zoezi la uapisho uliofanyikia katika ukumbi wa wa Bogwe Sekondari katika Halmashauri ya Mji Kasulu chini ya huku wakiombwa kufata misingi ya kiuongozi.
Uapisho huo umefanyika Novemba 29 chini ya hakimu Mwandamizi Rajabu Fakihikutoka mahakama ya Mwanzo Kasulu Mjini kabla ya Kiapo amewasihi kuendelea kushirikiana na mahaka katika kutatua changamoto za madai kabla ya kufika mahaakamani.
Aidha Mkurugenzi mtendaji katika wilaya ya Kasulu Dkt. Semistatus Mashimba amewapongeza viongozi hao kwa nafasi waliyochaguliwa huku akiwasihi kufanya kazi na kuacha tofauti za kisiasa bali kuwasaidia wananchi waliopo katika maeneo yao ya kazi.
Kwa upande wao baadhi ya wiongozi wa kata mbalimbali wameelezea namna watakavyo shirikiana na wananchi kutimiza majukumu yao huku wakitoa wito kwa wananchi kuwapa ushirikiano katika kutekeleza maajukumu yao.
Ifahamike kuwa zoezi la uapisho limefanyika mara baada ya zoezi uchaguzi wa serikali za mitaa ulifanyika Novemba 27 kutamatika na kuwapata viongozi wawakilishi katika Ngazi ya serikali za mitaa katika kata zote nchini.
