Kuhusu sisi

Radio Tadio

Radio Tadio ni jukwaa la usambazaji wa habari kutoka redio za kijamii zilizopo Tanzania Bara na Zanzibar lililoanzishwa rasmi mwaka 2020 likijumuisha zaidi ya vituo vya redio 40 vinavyochapisha habari kila siku.

Mpaka sasa tuna vituo vya redio wanachama zaidi ya 40 pote Tanzania Bara na Zanzibar. Vituo hivi vya redio vinarusha matangazo na kufikia zaidi ya asilimia 70 ya eneo la Tanzania na kufikia mamilioni ya wasikilizaji nchini.

Tadio inatarajia kuendeleza ushirikiano na mashirika ya maendeleo, taasisi za serikali, mashirika ya kiraia na kampuni binafsi zinazopenda kufikia jamii ya vijijini kupitia redio za jamii kwa kufadhili vipindi au matangazo ya kulipia.

Kupitia jukwaa hili, redio washirika huchapisha habari, picha, vipindi na kurusha matangazo ya moja kwa moja. Habari nyingi zimejikita katika masuala mbalimbali ya jamii za vijijini hasa katika kilimo, ufugaji, afya, elimu, mazingira, jinsia, vijana, wazee, watoto na mengineyo mengi.

Lengo letu ni kuwa jukwaa linalotembelewa na idadi kubwa ya watumiaji kwa ajili ya kupata taarifa na mijadala inayohusu masuala ya vijijini.

Asante kwa kutembelea jukwaa hili.

TADIO

Asasi ya Habari za Maendeleo (TADIO), hapo awali ikijulikana kama Mtandao wa Vyombo vya Habari vya Kijamii Tanzania (COMNETA), ni mtandao wa kutengeneza na kuzalisha habari hasa zenye maudhui ya kijamii nchini Tanzania. TADIO imesajiliwa chini ya Sheria Nambari 24 ya mwaka 2002 ya usajili wa mashirika yasiyo ya kiserikali (NGO).

Kwa sasa kuna redio 40 zinazozalisha vipindi vya kijamii na kurushwa nchi nzima (Tanzania Bara na Tanzania Visiwani).

Ofisi zetu zinapatikana makao makuu ya Chuo Kikuu Huria Tanzania maeneo ya Kinondoni, Dar es Salaam ambapo pia tuna studio zetu za uzalishaji wa vipindi.

Unakaribishwa sana na pia unaweza kuwasiliana nasi kushirikiana katika miradi mbalimbali yenye lengo la kuiwezesha jamii ya watu waliopo vijijini na Tanzania kwa ujumla. Kwa habari zaidi, tembelea tovuti ya TADIO hapa.