Smile FM Radio

Kuelekea siku ya wanawake Manyara

March 6, 2026, 1:46 pm

Picha ya Afisa maendeleo ya jamii na mratibu wa dawati la mtambuka Halmashauri ya mji wa Babati, Ivetha Qamara Qawoga

Wanawake wametakiwa kutokutumia 50 kwa 50 vibaya kwa kutokutimiza majukumi yao

Na Kudra Massaga

Kuelekea siku ya wanawake duniani machi 08 , wanawake Mkoa wa Manyara wametakiwa kulea familia zao ili kujenga mahusiano mazuri katika ngazi za familia na jamii kwa ujumla.
Hayo yamesemwa na Afisa maendeleo ya jamii na mratibu wa dawati la mtambuka Halmashauri ya mji wa Babati,Ivetha Qamara Qawoga wakati akiwa kwenye mahojiano ya kipindi cha Tubonge kinachorushwa na Smile fm Radio
Amesema ni muhimu wanawake kuzitambua nafasi zao katika familia licha ya kuwa na shughuli nyingine za utafutaji

Sauti ya Afisa maendeleo ya jamii na mratibu wa dawati la mtambuka, Ivetha Qamara Qawoga

Hata hivyo Bi. Ivetha amesema suala la malezi linahitaji ushirikiano wa baba na mama na kuwataka wanaume kushurikiana na wanawake kwenye kulea na sio kutoa matunzo pekee.

Sauti ya Afisa maendeleo ya jamii na mratibu wa dawati la mtambuka, Ivetha Qamara Qawoga

Siku ya wanawake duniani mwaka huu imebebwa na kauli mbiu isemayo ‘haki na usawa kwa wanawake na wasichana , msingi jumuishi kufikia dira 2050’ na kwa Mkoa wa Manyara maadhimisho hayo yatafanyika katika Wilaya ya Simanjiro na mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mkuu wa Mkoa Queen Sendiga.