Smile FM Radio

Wananchi watakiwa kuwalinda na kuwahifadhi wanyama

March 5, 2026, 1:45 pm

Picha ya Afisa wanyamapori Halmashauri ya Babati, Goodluck James

Ikiwa tarehe 03 machi ilikuwa ni siku ya wanyamapori duniani wananchi wamekumbushwa kuwalinda wanyama

Na Kudra Massaga

Wananchi wametakiwa kusaidiana na wahifadhi wa wanyamapori katika kuwatunza na kuwahifadhi ili wazidi kuendelea kuwepo kwa kizazi cha sasa na cha baadae kwani wana faida katika uchumi kwa pato la mtu mmoja mmoja pamoja na taifa kwa ujumla.
Hayo yamezungumzwa na Afisa wa wanyamapori Halmashauri ya wilaya ya Babati Mkoa wa Manyara Goodluck James wakati akiwa katika kipindi cha tubonge kinachorushwa na smile fm radio

Sauti ya Afisa wanyamapori Goodluck James

Ikumbukwe kila tarehe 03 machi kila mwaka dunia huadhimisha siku ya wanyamapori duniani , ambapo amesema kuna changamoto nyingi ambazo huwa zinawakumba wanyama ikiwemo mabadiliko ya tabia nchi, magonjwa pamoja na ujangili

Sauti ya Afisa wanyamapori Goodluck James

Mkoa wa Manyara ni miongoni mwa mikoa ambayo iko na hifadhi za wanyamapori, ambapo mara nyingi wanyama huingia kwenye makazi ya watu pamoja na kufanya uharibifu wa mazao, kutokana na hilo Afisa huyo ameweza kuzungumzia ni utaratibu upi unatakiwa kufuatwa na wananchi ikiwa wanyama wamefanya uharibifu.

Sauti ya Afisa wanyamapori Goodluck James