Smile FM Radio

Manyara hali ni shwari zoezi la upigaji kura

October 29, 2025, 12:35 pm

Picha ya mkuu wa mkoa wa manyara Queen Sendiga akiwa tayari amepiga kura

Wananchi wilaya ya Babati wamejitokeza katika vituo vyao walivyojiandikishia kwa ajili ya zoezi la kupiga kura

Na Linda Moseka

Mkuu wa Mkoa wa Manyara Queen Sendiga mapema leo ameongoza wananchi katika zoezi la kupiga kura ili kuchagua viongozi kuanzia ngazi ya Raisi, wabunge na madiwani ikiwa ni sehemu ya kutimiza takwa la kikatiba.

Akizungumzia hali ya usalama akiwa kama mwenyekiti wa kamati ya usalama mkoa wa Manyara Sendiga amesema mpaka sasa hali ni shwari kwenye vituo vyote na wananchi wanaendelea kujitokeza kwa wingi.

Sauti ya Queen sendiga mkuu wa mkoa wa Manyara

Aidha sendiga ameongeza kuwa ameendelea kupokea taarifa na picha mbalimbali kutoka maeneo tofauti ya mkoa kama Kiteto, Simanjiro ,Mbulu ,Hanang’ kuwa saa moja kamili watu walishafika kwenye vituo huku akitoa rai kwa wananchi wa Manyara ambao bado wapo nyumbani wasihofu kwakuwa bado hawajachelewa kwani zoezi lipo mpaka saa kumi jioni vituo vitakapofungwa.

Sauti ya Queen sendiga mkuu wa mkoa wa Manyara