Smile FM Radio

80,910 kupiga kura jimbo la babati mjini

October 28, 2025, 2:17 pm

Picha ya msimamizi wa uchaguzi jimbo la Babati Mjini Simon Mumbee

Wananch wametakiwa kufanya uhakiki mapema wa majina kwenye vitio walivyojiandikishia kabla ya kuingia kwenye vyumba vya kupigia kura tarehe 29 oktoba 2025

Na Kudra Massaga

Jumla ya wapiga kura 80,910 wanatarajiwa kupiga kura kwenye vituo 206 ambavyo vipo katika kata nane jimbo la babati mjini mkoani manyara.
Hayo yamebainishwa na msimamizi wa uchaguzi kwenye jimbo hilo Simon Mumbee wakati akizungumza na wananchi kupitia kipindi cha TUBONGE kinachorushwa na SMILE FM RADIO.
Mumbee amesema kwenye vituo vya kupigia kura tayari orodha ya wapiga kura imebandikwa pamoja na orodha ya wagombea wa urais, ubunge pamoja na udiwani katika kata husika.

Sauti ya msimamizi wa uchaguzi Babati Mjini Simon Mumbee
Afisa uchaguzi babati mjini Bashan Kinyunyu amesema mambo muhimu kwa mpiga kura ni pamoja na kuwa na utayari wa kushiriki zoezi hilo pamoja na kuwa na kitambulisho cha kupigia kura au kitambulisho mbadala ambacho kimeruhusiwa na tume.

Sauti ya afisa uchaguzi jimbola Babati mjini Bashan Kinyunyu

Zoezi la kupiga kura litafanyika kesho tarehe 29, oktoba 2025 , ambapo wananchi wa tanzania watapata wasaa mwingine wa kuchagua viongozi kwa ngazi ya uraisi, ubunge na udiwani watakao waongoza kwa kipindi cha miaka mitano ijayo,