Smile FM Radio
Smile FM Radio
October 27, 2025, 2:43 pm

Picha ya viongozi wa jumuiya ya maridhiano na amani mkoa wa Manyara wakiwa kwenye maombi maalim ya kuliombea Taifa kuelekea uchaguzi mkuu
Kumefanyika mkutano wa kuliombea Taifa la Tanzania ili amani izidi kudumu hasa kwa kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu
Na Kudra Massaga
Jumuiya ya maridhiano na amani Tanzania kwa mkoa wa Manyara imefanya dua maalum ya kuliombea taifa katika kipindi hiki muhimu cha kuelekea uchaguzi mkuu utakaofanyika tarehe 29, octoba 2025.
Akizungumza leo katika mkutano uliowakutanisha viongozo wa dini, wadau wa jumuiya hiyo pamoja na waandishi wa habari katika ukumbi wa white rose uliopo Babati mjini, katibu wa maridhiani na amani mkoani humo Bishop Josiah sumaye amesema hiki ni kipindi muhimu kwa waumini na viongozi kuliombea taifa letu ili amani iendelee kudumu maana viongozi wana nafasi kubwa mbele za mungu.
Sauti ya katibu wa maridhiani na amani mkoani humo Bishop Josiah sumaye
Kwa upande wake mjumbe wa halmashauri kuu ya taifa maridhiano Juma Mkola Mnec nia ya kukufanya maombi hayo ni kubadilisha mawazo ya kila ambae alikuwa na agenda tofauti na uchaguzi aweze kurudi kwenye mstari na kushiriki kwenye zoezi hili muhimu la kupiga kura.
Sauti ya Mjumbe wa Halmashauri kuu ya Taifa maridhiano Juma Mkola Mnec
Pia Mnec ametumia fursa hiyo kuwaasa viongozi wa dini wasijiingize kwenye masuala yasiyofaa badala yake wawaelekeze waumini wao jinsi ya kupiga kura ili kutafuta viongozi wao wa kuwaongoza.
Sauti ya Mjumbe wa Halmashauri kuu ya Taifa maridhiano Juma Mkola Mnec
Nae makamu mwenyekiti wa JMAT Wilaya ya Babati NUHU IBRAHIM amesema kila kiongozi na wadau wazidi kuihubiri amani nchini.
Sauti ya Makamu mwenyekiti wa JMAT Wilaya ya Babati NUHU IBRAHIM
Kwa upande mwingine wajumbe walioshiriki mkutano huo wamesema wamefarijika kwa kukutana pamoja na kufanya dua hiyo muhimu kwa taifa letu.
Sauti ya maadhi ya wajumbe walioshiriki mkutano huo