Smile FM Radio

Vitambulisho mbadala kwa waliopoteza vitambulisho vya kura kutumika

October 21, 2025, 2:39 pm

Picha ya msimamizi wa uchaguzi Jimbo la Babati Simon Mumbee

Vitambulisho vyenye taarifa sahihi na zilizokuwepo kwenye kitambulisho cha kupigia kura vitatumika kwa wale waliopoteza

Na Kudra Massaga

Msimamizi ya Uchaguzi Jimbo Babati Mjini Simon Mumbee amesema wananchi wote waliojiandikisha katika dafatari la kudumu la wapiga kura la Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi kuwa mpiga kura na kupoteza kadi kwa bahati mbaya, wataruhusiwa kupiga kura endapo watafika kwenye vituo walivyojiandikisha wakiwa na vitambulisho mbadala vikiwa na jina linalofanana na lililomo kwenye dafatari la kudumu la mpiga kura.

Mumbee ameeleza hayo wakati Akizungumza na waandishi wa habari kuelekea siku ya uchaguzi mkuu Kwamba kwa mujibu wa kifungu Cha 69 (1) Cha Sheria ya Uchaguzi wa rais wabunge na madiwani namba 1 ya mwaka 2024, uchaguzi wa rais wabunge na madiwani utafanyika octoba 29 mwaka huu siku ya jumatano, hivyo kwa yeyote aliyejiandikisha kuwa mpiga kura ni lazima afikie na kitambulisho chake ili kupata nafasi na kupiga kura na kwa wale walio poteza vitambulisho wataruhusiwa kwa kua na vitambulisho mbadala vinavyo fanana na majina yaliyopo kwenye daftari la kudumu.

Sauti ya msimamizi wa uchaguzi Jimbo la Babati Mjini

Aidha amebainisha kuwa vituo vya kupigia kura vitakuwa sawa na vile vilivyotumika wakati wakuandikisha wapiga kuru ambapo vitafunguliwa saa moja kamili asubuhi na kufungwa saa kumi kamili Jioni lakini kwa vituo vya magereza vitafunguliwa saa mbili asubuhi na kufungwa saa tisa alasiri huku akitoa rai kwa wananchi kujitokeza kwa wingi kupiga kura siku hiyo ya jumatano October 29.

Sauti ya msimamizi wa uchaguzi Jimbo la Babati Mjini