Smile FM Radio

“wananchi jitokezeni kutimiza takwa la kikatiba”

October 20, 2025, 2:38 pm

Picha ya mkuu wa wilaya Emanuela Mtatifikolo kaganda

Kuelekea uchaguzi mkuu wananchi Wilaya ya Babati wametakiwa kwenda kupiga kura ili kutimiza haki yao ya msingi

Na Kudra Massaga

Wito umetolewa kwa wananchi wa Wilaya ya Babati Mkoani Manyara kujitokeza kwa wingi kwenye zoezi la kikatiba la kupiga kura litakalofanyika tarehe 29 octoba 2025.
Akizungumza na waandishi wa Habari Ofisini kwake Mkuu wa Wilaya ya Babati Emanuela Kaganda amesema ni muhimu kwa kila mtanzania ambae amefikisha umri wa miaka 18 na kuendelea na mwenye sifa ya kupiga kura aweze kushiriki zoezi hili muhimu.

Sauti ya mkuu wa wilaya ya Babati

Mh Kaganda amesema ili nchi iweze kuendelea kupata maendeleo ni kwa kupata viongozi ambao wataweza kuyafanya hayo sambamba na kudumisha amani na utulivu ndani ya nchi yetu.

Sauti ya mkuu wa Wilaya ya Babati

Kwa upande wa usalama, kaganda amesema kamati ya usalama ya wilaya wamejipanga kwa ajili ya kulinda wananchi na mali zao katika kipindi chote cha uchaguzi.

Sauti ya Mkuu wa Wilaya ya babati